Dodoma: Mahakama Kuu yatupilia mbali shauri la mapitio kuhoji Uhalali wa Mawakili kuwatetea waliombaka Binti wa Yombo

Dodoma: Mahakama Kuu yatupilia mbali shauri la mapitio kuhoji Uhalali wa Mawakili kuwatetea waliombaka Binti wa Yombo

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma imetupilia mbali kwa mara nyingine shauri la mapitio ya mwenendo wa kesi ya jinai inayowakabili washitakiwa wanne wanaodaiwa kumbaka kwa kundi na kumwingilia kinyume cha maumbile binti, mkazi wa Yombo Dovya jijini Dar es Salaam.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya Mahakama kujiridhisha kuwa shauri hilo halina mashiko kisheria.
Shauri hilo namba 24889 la mwaka 2024 ambalo lilikuwa mbele ya Jaji Steven Kakolaki lilifunguliwa na wakili Leonard Mashabara kwa mara ya pili, baada ya Mahakama hiyo kulitupilia mbali kutokana na kuwapo kasoro za kisheria.
1726642907165.png

Mahakama ililitupa shauri la awali baada ya Mashabara kuwaingiza watu ambao hawahusiki kwenye kesi ya msingi inayoendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma kuwa wajibu maombi.

Uamuzi wa kwanza ulitolewa na Jaji Suleiman Hassan Agosti 29, 2024 kutokana na pingamizi lililowekwa na wajibu maombi wakieleza baadhi yao hawahusiki katika kesi ya msingi.

Waombaji ambao hawahusiki na kesi ya msingi ni Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Mwanasheria Mkuu wa Serikali na mawakili wanne wanaowatetea washitakiwa kwenye kesi ya msingi.

Baada ya uamuzi huo wa Mahakama, Mashabara kupitia wakili wake Emmanuel Anthony walifungua shauri lingine mahakamani hapo dhidi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali na washitakiwa wanne wanaoshitakiwa kwenye kesi ya msingi iliyopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma.

Soma: =>
 
Wakili Mashabara anakwama wapi?

Uzembe huo utasababisha huyo binti akose haki yake.

Mahakama inafuata ukweli wa Kisheria ingawa kuna ushahidi wa kutosha (kama vile video iliyorekodiwa) dhidi ya washitakiwa lakini uamuzi wa mahakama unategemea sheria na taratibu za kisheria. Ikiwa kesi imejaa dosari za kisheria inaweza kutupiliwa mbali kwa msingi huu.
 
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma imetupilia mbali kwa mara nyingine shauri la mapitio ya mwenendo wa kesi ya jinai inayowakabili washitakiwa wanne wanaodaiwa kumbaka kwa kundi na kumwingilia kinyume cha maumbile binti, mkazi wa Yombo Dovya jijini Dar es Salaam.
Serikali imeharibu kwa kufanya makosa ya kiufundi kwa makusudi

Watanzania, sasa mjilinde na mjitwalie haki pale inapobidi
 
Wakili Mashabara anakwama wapi?

Uzembe huo utasababisha huyo binti akose haki yake.

Mahakama inafuata ukweli wa Kisheria ingawa kuna ushahidi wa kutosha (kama vile video iliyorekodiwa) dhidi ya washitakiwa lakini uamuzi wa mahakama unategemea sheria na taratibu za kisheria. Ikiwa kesi imejaa dosari za kisheria inaweza kutupiliwa mbali kwa msingi huu.

Mimi ni mmoja wa watabiri wa kusema kwamba hawa watuhumiwa wataachiwa kutokana na udhaifu wa ushahidi, lakini kuna wale waling'ang'ana kwamba video ipo.

Video siyo ushahidi mzuri kwa sababu una vipengele vingi na hata hivyo, muda ulikuwa umeenda sana kiasi kwamba ikawa vigumu kutambua ni uume wa nani uliingia maungoni mwa Binti.
 
Nilipoona tu madeleka, tls na wapinzani wameingilia hii kesi nikajua hamna kitu hapa
sure,
umefikiria kama navyofikiria.

always,
kwenye kesi za maana akionekana huyo sijui mandelenka na hao wengine ulowataja basi, ujue ni mihemko tu hakuna kesi hapo ,

watu wanadhalilika na kupoteza haki zao tu 🐒
 
Back
Top Bottom