Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma imetupilia mbali kwa mara nyingine shauri la mapitio ya mwenendo wa kesi ya jinai inayowakabili washitakiwa wanne wanaodaiwa kumbaka kwa kundi na kumwingilia kinyume cha maumbile binti, mkazi wa Yombo Dovya jijini Dar es Salaam.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya Mahakama kujiridhisha kuwa shauri hilo halina mashiko kisheria.
Shauri hilo namba 24889 la mwaka 2024 ambalo lilikuwa mbele ya Jaji Steven Kakolaki lilifunguliwa na wakili Leonard Mashabara kwa mara ya pili, baada ya Mahakama hiyo kulitupilia mbali kutokana na kuwapo kasoro za kisheria.
Mahakama ililitupa shauri la awali baada ya Mashabara kuwaingiza watu ambao hawahusiki kwenye kesi ya msingi inayoendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma kuwa wajibu maombi.
Uamuzi wa kwanza ulitolewa na Jaji Suleiman Hassan Agosti 29, 2024 kutokana na pingamizi lililowekwa na wajibu maombi wakieleza baadhi yao hawahusiki katika kesi ya msingi.
Waombaji ambao hawahusiki na kesi ya msingi ni Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Mwanasheria Mkuu wa Serikali na mawakili wanne wanaowatetea washitakiwa kwenye kesi ya msingi.
Baada ya uamuzi huo wa Mahakama, Mashabara kupitia wakili wake Emmanuel Anthony walifungua shauri lingine mahakamani hapo dhidi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali na washitakiwa wanne wanaoshitakiwa kwenye kesi ya msingi iliyopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma.
Soma: =>