Dodoma: Mahakama ya Rufaa kusikiliza maombi ya CHADEMA kutaka kesi ya mgawanyo wa mali kufanyiwa marejeo

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Leo Machi 24, 2026 Mahakama ya rufaa itaanza kusikiliza maombi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ya kutaka yafanyike marejeo (revision) ya mwenendo wa kesi ya mgawanyo wa mali za Chama iliyofunguliwa na Saidi Issa Mohamed na wenzake wawili.

Ikumbukwe kuwa, Chadema kupitia kwa mawakili wake kilimuandikia barua Jaji Mkuu wa Tanzania kumuomba yafanyike marejeo baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa kesi hiyo kama inavyoendeshwa na Jaji Mwanga kwenye mahakama kuu masijala ya Dar es Salaam ambapo huko nyuma Chama hicho kiliwahi kumtaka Jaji Mwanga ajizulu kuendesha kesi hiyo baada ya kutilia shaka uendeshaji wake, jambo ambalo Jaji huyo alilikataa.

Kesi hii itasikilizwa chini ya jopo la Majaji watatuWanachama na Viongozi mbalimbali wa Chadema wanaendelea kuwasili Mahakamani hapa.

Jambo
 
Who are the judges?( Of appeal)
 
JF ya sasa, si msaada tena kama miaka mingi iliyopita. Miaka ile, matukio muhimu yatokeayo kila kona, tulikuwa tunahabarishwa LIVE, hivyo kujua kwa ukaribu matukio kadhaa kwa wakati. Mikutano ya CCM ,yule sijui Mwanadiwani alikuwa anahabarisha kila tukio kwa wakati. Na vyama vingine hivyo hivyo. Huko mahakamani, tuliopo mbali, tulikuwa kama nasi tupo ndani yake. Leo hii, utasubiri sana.
 
Mimi sijaelewa, yaani case ya Mali kivipi? Kuna watu wanawadai Chadema au vipi?
Au Kuna watu wanataka wapewe urithi wao mapema?
Na kama ni hivyo si muwaulize mnataka Nini na Nini kama kipo ndani ya uwezo wenu wapeni tu, Mali inatafutwa. Kuliko kuwa na mlolongo wa case nyingi mahakamani. Kumbuka Lissu bado tunamuombea Mungu atoke aje ayaongoze haya mapambano
 
Kesi inasema hakuna mgao sawia wa mali za chadema kati ya zanzibar na bara. Na aliyefungua kesi ni makamu mwenyekiti mstaafu ambaye amefungua kesi baada ya kushindwa uchaguzi.

Sasa kisheria chama ni kimoja hakunaga chadema zanzibar na chadema bara otherwise Tanganyika nao wataibuka wadai mali zao sasa hapo itakuaje!!

Chama ni kimoja so zanzibar inakua treated kama tu kanda zingine zote so kimsingi chadema hakidaiwi na mtu bali mtu anadai mgao uwe sawa mfano ikija ruzuku basi iwe 50-50 and so on!!

Sasa hapo unakubali nini? Kumbuka kesi ya msingi ni kama haijaanza na chadema imewekewa pingamizi isifanye siasa. Sasa hiyo kesi ikija kuisha 2030 itakuaje? Maana hata ikitoka hukumu bado mshindi ni chadema maana itaambiwa tu igawe mali equally. Ila hii kesi imewekwa kusogeza muda tu ili chama kifungiwe na ndio hasa kimewafanya waende dodoma ila bila hivyo wangekua wameitana mezani wayamalize
 
Hivi wewe unaamini kwamba hii kesi ni ya mgawanyo wa mali za chama kweli? Kesi ya mgawanyo wa mali ina uhusiano gani na uhuru wa wanachama wa kufanya shughuli za kisiasa?
 
Nimeelewa sasa, hii case imekaa kimkakati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…