Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 819
- 1,093
Mgombea wa Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa chama hicho na Mwenyekiti wa CHAUMMA Mkoa wa Dodoma, Aisha Madoga, amerejesha fomu ya kugombea ubunge katika Jimbo hilo leo Agosti 27, 2025.
Madoga na wagombea wengine kutoka vyama saba tofauti, wameteuliwa rasmi kugombea jimbo hilo baada ya kukidhi vigezo na masharti yanayotakiwa kwa mujibu wa sheria.
Zoezi hilo limefanyika mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dodoma Mjini, Wakili Cosmas Nsemwa.