Dodoma: Mradi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato umefikia kiwango cha asilimia 18.5

Dodoma: Mradi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato umefikia kiwango cha asilimia 18.5

DodomaTZ

Member
Joined
May 20, 2022
Posts
84
Reaction score
118
Mradi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato upo Kilometa 10 kutoka katikati ya Jiji la Dodoma, ulianza Aprili 20, 2022 baada ya mkataba kusainiwa Septemba 2021.

Mhandisi wa Miradi wa TANROADS Dodoma, Colman Gaston anasema mradi huo umefadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).
Uwanja wa Msalato (1).jpg

Uwanja wa Msalato (2).jpg
Unatekelezwa na Mkandarasi kutoka China, ukiwa unahusisha sehemu ya kurukia ndege, sehemu za kuegesha ndege, pia kuna uzio na miundombinu mingine ya umeme na moto.

Anasema hatua iliyofikiwa ni Asilimia 18.5 wakati ambapo katika mipango iliyowekwa ilipangwa hadi kufikia wakati huu iwe imefikia hatua ya 18.6%

Ameongeza kuwa: “Tunatarajiwa utakamilika Aprili 2025 kwa kiwango cha 100%.”

Mhandisi Gaston anafafanua kuwa Ujenzi wa Mradi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato utakuwa na sehemu ya pili ambayo inahusisha ujenzi wa jengo la abiria na mnara wa kuongozea ndege.

Kuhusu gharama za mradi kwa ujumla zinatarajiwa kuwa ni Tsh. Bilioni 194 kwa kuhusisha majengo na sehemu ya kuongozea ndege na kuwa mradi unatarajiwa kutumia miezi 36 hadi kukamilika kwake.
Mhandisi COLMAN Gaston-TANROADS.jpg
Ameeleza kuwa mara baada ya kukamilika kwa mradi, uwanja huo unatarajiwa kuhusisha ndege za kimataifa na za ndani na unatarajiwa kuwa na manufaa makubwa kwa Taifa hasa katika kukuza uchumi na maendeleo ya kijamii.
 
Back
Top Bottom