denooJ
JF-Expert Member
- Mar 31, 2020
- 18,509
- 68,228
Salaam,
Taarifa nilizozipata hivi punde toka chanzo changu kinanihabarisha kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman A. Mbowe amevamiwa na kikundi cha watu wasiojulikana akielekea nyumbani kwake usiku huu na kupigwa na wamemuumiza.
Tukio hili limetokea majira ya saa 6-7 usiku.
Mhe. Mbowe amekimbizwa Hospitali ya Ntyuka iliyopo jijini Dodoma.
Kamanda Muroto amesema wamepata taarifa kuwa kavunjwa mguu wa kulia na amelazwa Wodi namba 4 hospitalini hapo. Amesema taarifa zaidi zitafuata
UPDATES
FREEMAN MBOWE AHAMISHIWA DAR KUTOKEA DODOMA
Kiongozi huyo wa Kambi rasmi ya Upinzani, ametolewa katika hospitali ya DCMC jijini Dodoma na kusafirishwa kwenda jijini Dar kwa matibabu zaidi
Mnadhimu wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, Esther Bulaya amesema wataeleza baadaye ni hospitali gani anakwenda kutibiwa Mbowe, akifika jijini Dar
Daktari anayemtibu amesema hali ya Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai inaendela vizuri ila ni maumivu bado yupo nayo kutokana na kuvunjika kwa mfupa wa mguu wa kulia
MAONI YANGU:
Mhe. Mbowe kuvamiwa na kupigwa eneo la Area D, jijini Dodoma, Mtaa wa Sengia; linalotajwa kuwa na ulinzi wa kutosha, kama ilivyotokea kwa Lissu kunaacha maswali mengi, je, hili linaweza kuwa limechochewa na Lissu kutangaza nia ya kugombea Urais wa JMT October 2020? Ni hasira au kitu gani? No one knows.
Bado najiuliza; hivi kama Taifa kwa tabia hizi za kihuni tunaelekea wapi? Hawa wanaojichukulia sheria mikononi kila siku wanafanya hivyo kwa kutumwa na nani? Matendo haya yataendelea kwa viongozi wa upinzani mpaka lini?
We need to wake up, better late than never.
PIA SOMA
- Uelewa wangu juu ya kundi la watu wasiojulikana
~ Matukio ya Watu kupotea na wengine kudaiwa kutekwa, nini kinaendelea kuhusu usalama wa raia
- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana