Dodoma: Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe avamiwa, apigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana

Kwahiyo nchi yetu ni dhaifu kiulinzi?
 
Kweli kabisa, Na hii issue itaishia hewani tu
 
Wengine wanasema alikuwa kwa kimada sasa jamaa ake likamfumania
 
Wewe ni mjinga tu, usinifundishe chochote; ukitaka soma, ukipenda acha, huna lolote wewe na wapuuzi wenzio humu ndani.

Mnajifanya vipofu kutokuona hali halisi, mnataka kuuaminisha umma Mbowe kashambuliwa na vibaka tu, narudia tena wewe na wenzako Englishlady, Mtazamo, Mzee Mwanakijiji, Ngabu ni wapuuzi.

Hao vibaka huwa wanawashambulia Chadema peke yao kwa nini? kuanzia Alphonce Mawazo, Lissu, diwani kule Iringa, na wengine...

Kama ni vibaka tu wa hayo matukio kwanini hatuoni polisi hata wakiwakamata wahusika, hivi nyie ni vipofu wa aina gani mliozoea kuona damu ya wapinzani inamwagika halafu mnaendelea kuleta upuuzi wenu hapa?

Kama polisi wanashindwa kuwakamata hao watu, mnataka tuamini vipi tofauti? kwanini hao vibaka hawawezi hata mara moja kuwashambulia na viongozi wa CCM nao tuone?

Msitake kuleta ustaarabu wenu wa kijinga wa maigizo usio na maana, nyie ndio mnaoleta siasa za kipuuzi, mnataka kutuaminisha ni vibaka wasiokamatwa siku zote, mnaleta hisia zenu za "vita ya ndani ya kwa ndani", hiyo vita ya ndani ndio ilisababisha Mawazo afe? nyie ni wapuuzi, kama ni hivyo kwanini polisi hawawakamati hao wahalifu?

Nyie ni wanafiki, wenye malezi ya kinafiki.
 
Vizuri umekiri kuwa nchi yetu ina ulinzi dhaifu.
 
Huu ushenzi sasa hauvumiliki hata kidogo, sijui aliyehuska lakni bila ya kukamatwa aliyehuska akiri zetu ni lazima lawamazote ni Kwa serikali hasa katika swala zima la ulinzi

Narudia tena, wanajaribu upole wetu ambao pia ulishagafika mwisho, tunataka waliohuska wote wamekamatwa kama ilivyokuwa Kibiti na maeneo mengine yaliyowahi kuwa na majaribio ya kuvunja Amani nchini mwetu

La sivyo, vyombo vya ulinzi sasa wanatulazimisha kuichukia serikali
 
Aisee...

Jr[emoji769]
 
Bado itatokea sana if we dont wake up..Tuendelee kufundishwa adabu hivi hivii hadi akili zikae sawa..The psycopath is still leading the nation...Ndiye ambae hashtuki hata na lolote...
 
Inasikitisha sana na tabia hii ya kushambulia wapinzani haikubaliki pole mh mbowe
 
Najaribu kutafakari na kuchambua kwa kina kwani kila inapofika nyakati za uchaguzi mtia nia ndani ya Chadema lazima aumie au hata kufariki.

Rejea Chacha Wangwe
Rejea Sakata la Zitto na Issue ya kutaka kupewa sumu
Rejea shambulizi dhidi ya Lissu
n.k
Mwaka huu kaumizwa Mbowe(Pole kwake sana)
Je, kuna mtu kalipa kisasi?
Lakini kuna jambo lazima lichunguzwe ndani ya Chama cha Chadema.
 
Mmh hizi si dalili nzuri kabisa kuelekea uchaguzi mkuu... Njia zote zimeshindikana sasa hii ya kuumizana ndio silaha yao ya mwisho iliyobaki.. KUKICHWA KUTAMBAZUKA... WAKATI SI MILELE...

Jr[emoji769]
Kama matendo yao yanapelekea "kupendwa" kama wanavyojinasibu kuwa ni watetezi wa wanyonge. Kwanini wahangaike hivi kuhakikisha wanatoa uhai wa viongozi wa upinzano hasa CHADEMA?.
 
Hii taarifa ina ukakasi sana Ila wanaosema pia saa nane usiku alikuwa anatoka wapi wajitafakari sio lazima mtu ulale usiku Hata kama sio mlinzi mfano mimi nalala masaa saba na naweza kuyalala muda wowote hata mchana na usiku nika remain awake whole night, Lakini KUB kweli na Chairman of Chadema halindwi kweli? Tena kwa title yake yuko under protection na Armed guys iweje vibaka wamvamie, Btw lissu nae katangaza nia masaa kadhaa yaliyopita wacha tuweke akiba ya maneno na tumsubiri mwalimu asie danganya ambae ni "MUDA"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…