Dodoma: Serikali yasitisha mradi wa ujenzi wa barabara ya mzunguko wa kati unaopita kata ya Nkuhungu

Sasa mkuu, bhasi wasingeruhusu Ardhi iliyopangwa kw ajili ya "Ring road" wananchi waiendeleze.
Naona wamekosea, sasa hitaji mbeleni likihitajika[emoji134] watavunja makazi ya watu?
Mradi ulikuwa mzuri, sijui waliositisha wameona nini?!?
Naungana na WEWE by 100%,They should protect and stands with plans for future generations,hapa ndipo wazungu wanapotushia.
 

Hii ni habari njema sana. Kwani kuna barabara za KIMKAKATI zaidi ambazo zingali zimetelekezwa. Kwani barabara kama hii:


iko katika hali gani?

Barabara za mijini nazo ziko katika hali gani?

Mafuriko ya kila leo mijini kwa ubovu wa barabara yameshapata ufumbuzi wowote?

Hata viwanja vya ndege Chatto, daraja la Busisi na mingi ya miradi ya mwendazake isiyokuwa na kujali vipaumbele ilipaswa kusitishwa.

Hongera mama Samia kwa uongozi wa vitendo. Matendo kuongea zaidi kuliko maneno.
 
Mama ameshafeli, atakuwa raisi wa kike wa hovyo aliyewahi kutokea.

Hii ring road ilikuwa kipaumbele wakati tuna barabara kuu katika hali hizi?


Au huko sasa kulisha kamilika?
 
Mwenye maono alijenga International Airport kijijini, naweza sema alikuwa na akili kama zako
 
Mkuu bado unakomaa na hi barabara? Hi barabara tender ishatangazwa kitambo sana (Nov 2020) na mkandarasi alishapatikana, shida ni nn tena?au na yenyewe ujenzi umesitishwa?

 

Mkuu mimi nakomaa na vipaumbele tu ikiwamo hii barabara. Ndiyo maana nikahitimisha bandiko langu na swali lile:

"Au huko sasa kulisha kamilika?"

Kwamba mkandarasi alishapatikana? Acha maneno weka Muziki! Mkandarasi aliyepatikana anakuja lini site? Lini anapanga kazi kumalizika? Jina la mkandarasi - ingependeza zaidi.

Kwa kumbukumbu zilizopo mwendazake zake alikuwa akiahidi ujenzi kamili wa barabara hiyo na kuwa pesa anazo. Hii ikiwa regularly and yearly tokea 2015 hadi alipotutoka bila kutuaga 2021 pasipo na la maana lolote kufanyika.

Huyu mkandarasi unaye msema anaanza lini hiyo kazi mkuu?
 
Nakusoma mtaalam unavyovichapa bakora visichana vya jf
 
Miradi ya Magufuli ilikuwa ya kupiga hela, Ring road ipo na Mama kasema atajenga sasa hiyo ya Kati ilikuwa ya Nini? Ndio maaana alitutengenezea Meli za kutuuwa kule Kyela

Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
 
Miradi ya Magufuli ilikuwa ya kupiga hela, Ring road ipo na Mama kasema atajenga sasa hiyo ya Kati ilikuwa ya Nini? Ndio maaana alitutengenezea Meli za kutuuwa kule Kyela

Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app

Itakuwa ilikuwa ni ya kupendezesha hiki kama lile daraja mbadala la salenda.
 
Ili tatizo ni sababu ya kuwa na miradi ya mtu na sio miradi ya wananchi ambayo kuanzishwa kwake inajumuisha wadau wote....

Mradi wako ni sawa kama tu pesa yote unatoa wewe..., huwezi kutumia pesa za kila mtu kufanya miradi yako, tukiendelea hivi itakuwa kila miaka kumi tunaanzisha miradi ya mtu na kuacha miradi mingine ya mtu (tutakuwa watu wa kuanzisha na kusitisha tu...)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…