VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Lile vuguvugu lililoanzishwa na Wajumbe Huru (WAHU) la kutaka Samwel John Sitta kuwa Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge la Katiba limefikia pazuri.Sasa,karibu kila Mjumbe anamtaja Sitta kwa hili au lile ilimradi tu kumuunga mkono. Mmoja wa viongozi wa WAHU amenidokeza kuwa tayari Sitta ameshapita mbele ya Wajumbe na wanachosubiri sasa ni chama chake cha CCM kuleta jina lake Bungeni kwa nafasi hiyo.
'Hapa tayari.Tunaisubiri CCM ituletee jina lake hapa kama mgombea.Unajua...mchakato wa kuwapata wagombea wa nafasi kama hizi huwa ni wa ki-chama zaidi. Wakituangusha katika hili,tutawaangusha katika mambo mbalimbali ya kichama' alisema kiongozi huyo wa WAHU bila ya kusema wataiangusha CCM katika mambo gani.
Kwa hali ilivyo hapa katika viunga vya Bunge la Katiba Dodoma, Sitta hana mpinzani. Kwa siasa za Tanzania lakini chochote chaweza kutokea. Na Wajumbe watalazimika kusimamia wanachokiamini. Vile watakavyoona inafaa. Yetu macho na masikio!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (sasa Dodoma)