Dodoma: Spika Tulia aitaka Serikali ifanye tathimini kuhusu mfumo wa uagizaji mafuta

Dodoma: Spika Tulia aitaka Serikali ifanye tathimini kuhusu mfumo wa uagizaji mafuta

Inakuwaje mazutu ya Transit yepewe kipaumbele wakati Nchi haina Mazutu?
 
SPIKA wa Bunge, Dk Tulia Ackson ametaka ifanyike tathmini ya mfumo mpya wa uagizaji mafuta nchini.

Ametoa kauli hiyo bungeni muda mfupi kabla ya kusitisha shughuli za bunge mchana leo Septemba 7, 2023 na kusema ni wakati mwafaka kwa serikali kufanya tathimini kwa mfumo huo wa uagizaji mafuta kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza.

Amesema haiwezekani mafuta yanapatikana kwa wiki mbili na baada ya hapo yanakuwa hayapatikani, kisha baada ya muda yananza kupatikana.

Amesema kama mfumo huo unaleta changamoto basi warejee katika mfumo wa zamani kwa kuboresha maeneo yaliyokuwa na changamoto, lakini kama mfumo wa sasa nao unaonekana ni sahihi basi waangalie maeneo yenye changamoto parekebishwe.
Tathimini ifanywe mara ngapi wakati kipindi cha JPM ilifanyika na utaratibu ukawekwa lakini baada ya kulala si mfanyabiashara au kiongozi aliendelea kuzingatia utaratibu huo.

Wanasiasa wabaya sana mlimweka kiongozi fulani hapo alipoingia tu akaanza kufumua kila kitu ili kutengeneza mazingira ya upigaji dili sasa mnataka kitu gani cha ziada wakati alitakiwa huyo mwanasiasa ashughulikiwe ipasavyo
 
Huo ni kama ushauri tu, wangekuwa wanafanya kazi yao ya kuisimamia serikali basi ingeundwa kamati ya bunge ya kuchunguza nini chanzo cha tatizo.

Baada ya hapo ingekuja na mapendeleo Bungeni kisha bunge lingeyapitisha kwa azimio rasmi la bunge. Ikiwa ni pamoja na kuitaka serikali iwawajibishe wahusika.

Alas, hatuna Bunge, tuna kundi la wanasiasa ambao kazi yao ni kupitisha kinacholetwa na serikali, kupigapiga meza na kuachia ushuzi baada ya kuvimbiwa chakula cha bure wanacholishwa kwa kodi za walala hoi.

Yale yote ambayo bunge halikuyapitisha ni kwasababu wanachi walipiga kelele. Yaani wanachi wanalazimika kufanya kazi ya Bunge.
Yaani wewe jamaa umemaliza kabisaaaa
 
Spika kwenye suala hili angekuwa mnyoofu na mwadilifu basi angeshasikia na kuweka tume kama Luhaga Mpina alivyowahi kupendekeza ndani ya Bunge na Hansard ipo Leo anaongea akifikiri watu tumesahau au anasahau kuwa tech ya Leo watu Wana Wanaweka Hansard zao kwenye simu?
Inasikitisha kuongea kwa hofu na bila uhakika wa anachoshauri 😪
 
Naona jamaa yake kaona akiomba kushauri atamuuzi aliyemteua kwaiyo kamtumia mkewe kufikisha ujumbe
 
Back
Top Bottom