LGE2024 Dodoma: Uchaguzi wahairishwa kwa sababu ya kifo cha mgombea wa CCM

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko ametangaza kuahirishwa uchaguzi kwa nafasi ya wajumbe mchanganyiko katika mtaa wa Mwangaza jijini humo kwa mujibu wa Kanuni NO. 21 (ii) ya Kanuni za Uchaguzi Mamlaka za Mitaa, ngazi ya miji kutokana na mgombea wa nafasi ya ujumbe kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) kufariki dunia siku ya tarehe 11 Novemba, 2024 baada ya uteuzi wa wagombea kufanyika.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari na viongozi wa vyama vya siasa jijini Dodoma, leo tarehe 21 Novemba, 2024 Dkt. Sagamiko amesema kutokana na kifo cha mjumbe huyo aliyekuwa akiitwa Christian Chawene, uchaguzi unafanyika katika mitaa 221 badala ya 222 kwa nafasi za wajumbe mchanganyiko na kwa mujibu wa kanuni hiyo inamtaka msimamizi msaidizi wa uchaguzi kuahirisha uchaguzi wa nafasi hiyo katika mtaa husika na chama cha siasa kilichotoa mgombea aliyefariki kitaweza kuwasilisha jina la mwombaji mwingine ndani ya Siku 40 tangu kuahirishwa kwa uchaguzi, ili hatua za uteuzi kwa mwombaji huyo zifanyike.

Soma pia: Dodoma: Wananchi wamkataa mgombea wa CCM wadai wamechoka kuonewa

Aidha, ametoa rai kwa vyama vya siasa kufanya uchaguzi kwa kuzingatia kanuni bila kutumia lugha za matusi, kashfa, rushwa au ubaguzi wakati huu wa kampeni.

Naye Zacharia Mwandumbya akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Dodoma amewasisitiza viongozi wa vyama vya siasa kuwaelimisha wananchi juu ya ubaya wa rushwa na kuepukana na wagombea ambao wanatumia rushwa kwani itapelekea kupata viongozi wasiofaa na wanaonufaisha matumbo yao.​

Chanzo: Jambo TV
 
Msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko ametangaza kuahirishwa uchaguzi kwa nafasi ya wajumbe mchanganyiko katika mtaa wa Mwangaza jijini humo kwa mujibu wa Kanuni NO. 21 (ii) ya Kanuni za Uchaguzi Mamlaka za Mitaa, ngazi ya miji kutokana na mgombea wa nafasi ya ujumbe kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) kufariki dunia siku ya tarehe 11 Novemba, 2024 baada ya uteuzi wa wagombea kufanyika.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari na viongozi wa vyama vya siasa jijini Dodoma, leo tarehe 21 Novemba, 2024 Dkt. Sagamiko amesema kutokana na kifo cha mjumbe huyo aliyekuwa akiitwa Christian Chawene, uchaguzi unafanyika katika mitaa 221 badala ya 222 kwa nafasi za wajumbe mchanganyiko na kwa mujibu wa kanuni hiyo inamtaka msimamizi msaidizi wa uchaguzi kuahirisha uchaguzi wa nafasi hiyo katika mtaa husika na chama cha siasa kilichotoa mgombea aliyefariki kitaweza kuwasilisha jina la mwombaji mwingine ndani ya Siku 40 tangu kuahirishwa kwa uchaguzi, ili hatua za uteuzi kwa mwombaji huyo zifanyike.

Aidha, ametoa rai kwa vyama vya siasa kufanya uchaguzi kwa kuzingatia kanuni bila kutumia lugha za matusi, kashfa, rushwa au ubaguzi wakati huu wa kampeni.

Naye Zacharia Mwandumbya akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Dodoma amewasisitiza viongozi wa vyama vya siasa kuwaelimisha wananchi juu ya ubaya wa rushwa na kuepukana na wagombea ambao wanatumia rushwa kwani itapelekea kupata viongozi wasiofaa na wanaonufaisha matumbo yao.

View attachment 3157859

Chanzo: Jambo TV
Na msipo acha dhuluma ataka wekwa ata kufa tena
 
Muwambie ccm waache kutoa Raushwa kwenye chaguzi mbalimbali.
 
Back
Top Bottom