The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya Zegele - Chikopelo yenye urefu wa kilomita 16, pamoja na ujenzi wa kalavati la Chikopelo, kumeleta faraja kwa wananchi wa vijiji vya Chikopelo na Zegele, wilayani Bahi, Dodoma. Mradi huu ni sehemu ya juhudi za Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kupitia Mradi wa RISE, unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, kwa lengo la kuondoa vikwazo vya barabara.
Pia soma Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze
Mwenyekiti wa Kijiji cha Chikopelo, Bwawani Sumaji Mahajile Majiwa, ameipongeza serikali kwa kuwaletea mradi huo, akieleza kuwa hapo awali walikuwa na changamoto kubwa ya usafiri, hasa watoto waliokuwa wakisafiri kwenda Shule ya Msingi Chikopelo na wananchi waliotegemea Zahanati ya Chikopelo, iliyoko upande wa pili wa Mto Chikopelo. Aidha, ameeleza kuwa barabara hiyo itasaidia wakulima wa nyanya na mboga mboga kusafirisha mazao yao kwenda sokoni kwa urahisi na gharama nafuu.
Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa TARURA Wilaya ya Bahi, Mhandisi Respick Malya, amesema mradi huo ulijumuisha ujenzi wa barabara pamoja na boksi kalavati la Chikopelo.