Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Dodoma Majengo wamegoma kuondoka kwenye soko hilo kwenda kwenye masoko mengine ya pembezoni kupisha ukarabari na badala yake wamehamishia biashara zao nje kuzunguka soko hilo kwa kile wanachodai wanahofia kunyang’anywa vizimba vyao wakati litakapokamilika pamoja na kulinda mitaji yao.
Jumla ya wafanyabiashara 1,797 na mabucha 51 ndiyo wanaotakiwa kupisha ukarabati huo huku wenyewe wakisema hawako tayari kuondoka nje ya maeneo yanayozunguka soko hilo linalokarabatiwa kwasasa kupitia mradi wa uboreshaji wa miji na majiji maarufu kama TACTIC.