PreGE2025 Dodoma: Wananchi walalamika Diwani wao kuwapiga, na kuwatoa vitisho pindi wanapodai maendeleo

PreGE2025 Dodoma: Wananchi walalamika Diwani wao kuwapiga, na kuwatoa vitisho pindi wanapodai maendeleo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Wananchi wa Kijiji cha Mlowa Bwawani, Wilaya ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma, wamemlalamikia Diwani wa kata hiyo, Andrew Richard Mseya (CCM), kwa madai ya kutumia mamlaka yake kuwanyanyasa, kuwapiga, na kuwatoa vitisho pindi wanapodai maendeleo katika kijiji chao.

Wakizungumza na waandishi wa habari, wakazi hao wamesema wananyimwa uhuru wa kutoa maoni yao, hasa kuhusu masuala ya maendeleo. Wamedai kuwa Diwani huyo huwafuatilia, kuwanyanyasa, na hata kuwapiga wanapozungumza kwa uwazi kwenye mikutano au kupitia majukwaa mbalimbali.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Kwa mujibu wa mmoja wa wakazi hao, Abdulaziz Aboubakar, tukio la hivi karibuni lilitokea baada yake kuuliza maswali kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia kundi la WhatsApp la kata hiyo. Anadai kuwa kitendo hicho kilimkasirisha Diwani, ambaye baadaye alimtishia na hatimaye kumfuata na kumpiga.

 
Yaani unapigwaje? na diwani, huyo huyo ambaye anakuja kuanza kupiga magoti akiomba kura?
 
Back
Top Bottom