Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Wakazi wa Mtaa wa Chinyoya, Kata ya Kilimani, Wilaya ya Dodoma Mjini, jijini Dodoma, wamepinga uteuzi wa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anayewania nafasi ya uenyekiti, wakidai kuwa mgombea huyo ameonesha tabia za kujifanyia maamuzi kwa matakwa yake binafsi na kutumia ubabe katika uongozi.
Wakiwa na waandishi wa habari mtaani hapo, wakazi hao wameeleza kuwa mwenyekiti huyo mteule amekuwa akiendeleza migogoro ya ardhi na kuchochea malalamiko kwa kutumia nafasi yake. Wameeleza kuwa hatua ya CCM kuteua mgombea huyo imewaumiza wananchi, na wanaona ni kama chama hakijazingatia maslahi ya wananchi wake.
Katika siku za karibuni, kumekuwepo na malalamiko mengine mkoani Dodoma kuhusu uteuzi wa wagombea wa serikali za mitaa kwa chama hicho, ambapo baadhi ya watia nia waliopendekezwa na wajumbe hawakurudishwa, na majina mapya yasiyochaguliwa yakipewa kipaumbele. Malalamiko haya yametokea pia katika wilaya za Mpwapwa na Chemba.