Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
JESHI la Polisi mkoa wa Dodoma limewakamata ndugu wanne wa familia moja wanaotuhumiwa kumuua ndugu yao na kisha kumkata miguu yote miwili chini ya magoti na kuufunika mwili kwa mahindi yaliyopukuchuliwa na kuuchoma moto.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Onesmo Lyanga alisema jana kuwa, watuhumiwa hao ni wakazi wa kijiji cha Daki, tarafa ya Mondo, wilaya ya Chemba, mkoani Dodoma.
Alimtaja aliyeuawa kuwa ni Rashid Nduata (40) na kwamba iligundulika aliuawa ndani ya nyumba yake.
Kwa mujibu wa Kamanda Lyanga, Nduata aliuawa kwa kunyongwa shingo, kuchomwa na kitu chenye ncha kali shavu la kulia, kupigwa na kitu kizito kwenye taya la juu na chini na kisha kukatwa miguu sehemu ya chini ya magoti.
“Mwili wake ulifunikwa na mahindi yaliyopukuchuliwa na kuchomwa moto,” alisema.
Alisema wanafunzi kijijini hapo walikuwa wakipita kando ya nyumba hiyo na kuona moshi ukitoka ndani na ndipo walitoa taarifa.
Kamanda Lyanga alisema chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa ardhi kati ya marehemu na ndugu zake. “Watu wanne wamekamatwa kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo,” alisema
HabariLeo