Dodoma: Watuhumiwa mauaji ya mtoto Graison wafikishwa mahakamani

Dodoma: Watuhumiwa mauaji ya mtoto Graison wafikishwa mahakamani

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Watuhumiwa wawili wanaokabiliwa na kesi ya mauaji ya mtoto wa Graison Kanyenye (6) wamefikishwa mahakamani jijini Dodoma leo Jumatatu, Desemba 30,2024.

Soma, Pia: Dodoma: Mtoto wa miaka 6 auawa kikatili na watu wasiojulikana
1735543356139.png

Mpaka sasa bado haijajulikana kesi hiyo itasomwa katika mahakama gani.

Graison, mtoto wa mfanyabiashara maarufu jijini hapa, Zainab Zengo maarufu 'Jojo' anadaiwa kuuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani wakati mama yake akiwa matembezini usiku wa kuamkia Desemba 25, 2024.

Watuhumiwa waliotajwa ni Kelvin Gilbert, dereva bodaboda, na Tumaini Msangi, ambaye ni bondia.
IMG_2135.jpeg
 
Watuhumiwa wawili wanaokabiliwa na kesi ya mauaji ya mtoto wa Graison Kanyenye (6) wamefikishwa mahakamani jijini Dodoma leo Jumatatu, Desemba 30,2024.

Soma, Pia: Dodoma: Mtoto wa miaka 6 auawa kikatili na watu wasiojulikana
View attachment 3188395
Mpaka sasa bado haijajulikana kesi hiyo itasomwa katika mahakama gani.

Graison, mtoto wa mfanyabiashara maarufu jijini hapa, Zainab Zengo maarufu 'Jojo' anadaiwa kuuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani wakati mama yake akiwa matembezini usiku wa kuamkia Desemba 25, 2024.View attachment 3188386
Ukichunguza kwa haraka haraka utagundua kwamba mkasa huu unahusiana na masuala ya Paternity Fraud.
Yawezekana huyo bodaboda na huyo mtuhumiwa mwingine watakuwa wameangushiwa jumba bovu tu huku Wahusika halisi wakiwa wapo huru uraiani.

Jeshi la Polisi Tz kwa kuwa liko completely incompetent, endapo kama lingekuwa competent enough Basi mpaka sasa mkasa huu ungekuwa tayari limeupatia suluhisho la uhakika la kisayansi kiasi kwamba Water tight evidences ungekuwa umeshapatikana, na watuhumiwa wasingekuwa na namna yoyote ile ya kuweza kukwepa kuwajibishwa kisheria kwa sababu Ushahidi uliopo ungekuwa umewabana Moja kwa moja.
 
Kumuua mtoto ni kosa lisilohitaji huruma ya aina yoyote ile.
Sayansi ya namna hiyo ni ngumu Sana kuipatia Maelezo yaliyo sahihi, hatujui bayana yaliyojificha nyuma ya pazia. You never know.

Kule nchini Rwanda miaka michache kabla ya kutokea kilele cha maua ya halaiki (Rwanda Genocide) mwaka 1994, kulikuwa na propaganda au kitu kilichoitwa kuwa ni "Ten Commandments of Hutu," Mojawapo ya hizo Ten Commandments of Hutu ilikuwa inasema kwamba "Kuua ni DHAMBI, lakini kumuua Mtutsi siyo Dhambi na Wala siyo Kosa kisheria, bali ni Kitendo cha Kishujaa cha Kujihami dhidi ya Adui hatari."
 
Mama mtoto anatajwa kama mfanyabiashara maarufu mjini Dodoma. Kwa biashara gani?

Hawa waandishi mbona wanaleta mazoea kwenye biashara, mtu anadanga ghafla mara anaitwa mfanyabiashara tena maarufu, tena jijini kabisa bora ingekuwa kijijini.
 
Back
Top Bottom