Dodoma: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa awaambia Mawaziri kuwa CCM itakwenda na mtu mmoja pekee ambaye ni Samia Suluhu Hassan

Dodoma: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa awaambia Mawaziri kuwa CCM itakwenda na mtu mmoja pekee ambaye ni Samia Suluhu Hassan

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mwaka 2025 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitampeleka kwa wananchi mtu mmoja, Rais Samia Suluhu Hassan hivyo mawaziri watambue hilo.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Oktoba 29, 2021 katika ukumbi wa St Gasper jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa mawaziri na naibu mawaziri.

Majaliwa amewataka mawaziri na naibu wao kuwa wasemaji wakubwa wa mafanikio ya Serikali ili itakapofika 2025, Samia Suluhu Hassan (Rais) apite na kusema kidogo tu.

"Wambieni wananchi kuhusu mazuri yanayofanywa na Serikali hii, tambueni msimamo na mtazamo wa Rais ili mkawe wasemaje zaidi yeye akija awe na maneno machache ya kueleza," amesema.

Waziri Mkuu amewataka mawaziri na naibu wao kufanya kazi kwa mashirikiano na kuheshimu kauli za viongozi wakuu kwani siyo kila agizo lazima waandikiwe barua ndipo watekeleze.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amewataka viongozi hao kuwa mfano kwa mienendo yao wakianzia na mavazi, kauli na kutojiinga katika mambo yatakayowafanya wajadiliwe.
 
Nampenda mama lakini inaonekana ccm bado hawajajifunza kitu kwa kifo cha mwendakuzimu.

Mungu ndiye anayejuwa kesho yetu, huenda yeye Majaliwa asifike 2025 au tukafika 2025 Rais akiwa ni Dr Mpango.

Waache hizi kufuru kwa sababu ya kiburi cha uzima.
 
EFF0680E-1D47-4E4A-BA4B-3D8CD245B67D.jpeg
 
  • Kicheko
Reactions: BAK
Hawa viumbe wanakera sana! Yaani kwao madaraka na utawala ndiyo vipaumbele vyao. Siku zote wanawazia matumbo yao tu na kutembelea Ma V8, huku wakiwaweka kwenye foleni walalahoi ili wapite kwa mbwembwe, na wakichagizwa na vile ving'ora vya policcm.
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mwaka 2025 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitampeleka kwa wananchi mtu mmoja, Rais Samia Suluhu Hassan hivyo mawaziri watambue hilo...
CCM utafikili Wana ahadi na MUNGU ,anajuaje Kama 2025 atakuwepo?

Mafanikio huwa yanatangazwa kwa wananchi katika Dunia ya sasa!

Mnafikili bado tupo Zama za mawe?
 
Hivi wewe unaposema mwendakuzimu huwa unamaanisha nini? Acha upumbavu wako! Wewe ni mkamirifu? Umejaa utaahira bichwa lako!
Namaanisha mwendakuzimu.

Halafu mimi huwa silali na deni, mpumbavu mamako kenge wewe.
 
Back
Top Bottom