Dodoma yaweza kuwa kama Windhoek

..mkuu acheni story za vijiweni...Nigeria yenye uchumi wa juu Africa ije ichukue ramani ya mji wa dom ambao hata haujajengwa?.ujinga sana πŸ˜†
 
Namibia nzima ina watu 2.5 milion unategemea mji uwe na watu wangapi. Jpili kama leo kuko kama Moshi hakuna mtu mjin.
 
Lilianza Abuja, lakini master plani ya Dodoma ilikwepo miaka mingi kabla ya abuja na ndipo wataalamu wa mipango miji kutoka Nigeria walikuja kujifunza Dodoma kipindi hicho
Ongeza nyama mkuu, ilikuwa lini? Umetetea hoja yako vizuri ila hujawa full of facts.
 
Windhoek siku za weekend unaweza ukalala barabaran nusu saa na usione gari ipite tena hapo ni katikati ya jiji kabisa, siku za weekend watu mjini ni wa kuhesabika mji unakuwa kimyaaa..Njoo sasa kwa upande wetu siku za weekend makelele tu ya Maamapiano kuanzia mitaa ya uhindini, Nkuhungu, Fourways vurugu tupu malaya kila kona
 
..mkuu acheni story za vijiweni...Nigeria yenye uchumi wa juu Africa ije ichukue ramani ya mji wa dom ambao hata haujajengwa?.ujinga sana πŸ˜†
stori zipi za vijiweni hujui kuwa Dodoma ilipewa hadhi/status ya makao makuu ya nchi tangu mwaka 1974.Hiyo Abuja imekuja kupewa hadhi ya mji mkuu wa Nigeria mwaka 1991 ...kabla ya hapo mji mkuu wa Nigeria ulikua Lagos baadae ndio wakahamisha kutoka Lagos kwenda Abuja mwaka 1991.Sababu za kuhamisha makao makuu ya nchi Nigeria kutoka Lagos kwenda Abuja zinafanana na za Tanzania kuhamisha makao makuu kutoka Dar kwenda Dodoma.
 
Wezi wa hela za serikali wale wapi?
Bajeti za usafi wa mazingira zipo ila pesa zinapigwa tu
 
..sasa mkuu kupewa hadhi ya kuwa makao makuu miaka ya zamani ndio kujengwa?..yaani wanaijeria walivyo highly educated waende kucopy ramani ya mji wa dom ambao haujajengwa kweli?.unawafahamu wanaijeria?umeshawahi kufika Abuja ukafananisha na dom?..yaani wanaija waache kwenda kujifunza&kuchukua ramani za majiji kama windhoek, capetown, Copenhagen, etc waende kuchukua ramani iliyotengenezwa na CDA dom kwa mji ambao haujajengwa?.acheni story za vijiweni!
 
Tatizo ni kuwa na population kubwa ya watu waharibifu kama watanzania. Windhoek ina watu wachache wanaojiheshimu.
 
..mkuu acheni story za vijiweni...Nigeria yenye uchumi wa juu Africa ije ichukue ramani ya mji wa dom ambao hata haujajengwa?.ujinga sana πŸ˜†
Wanaigeria walikuja kujifunza jinsi CDA ilivyopewa mamlaka ya kuendeleza jiji la Dodoma kuwa makao makuu. Naigeria nao walikuwa kwenye mipango ya kuhamisha makao yao makuu kutoka Lagos kwenda Abuja.

Wenzetu walikwenda kwenye utekelezaji moja kwa moja bila kusita wakati sisi tukikumbwa na kigugumizi hadi JPM alipoamua kulisukuma kwa nguvu zote.

Nchi nyingine iliyokuwa na mpango kama kwetu na wakautekeleza haraka ni Brazil ambapo walihamisha makao ya nchi yao kutoka Rio de Janeiro na kuijenga Brasilia.
 
This is Magufuli city DODOMA soon Dom tunakuwa kama MWANZA
 

Attachments

  • ice_2023-03-01-17-44-35-690.jpg
    919.7 KB · Views: 6
  • 20230622_193246.jpg
    391.3 KB · Views: 4
  • 20230204_143814.jpg
    696.4 KB · Views: 5

Wewe nawe unabisha ilimradi uonekane unabisha ...unapewa facts zote na bado unaendelea kubishana πŸ˜€πŸ˜€.
Ni hivi makao makuu ya Nigeria yalikua Lagos hadi mwaka 1991 walipohamishia Abuja katikati ya Nigeria(kama ilivyo kwa Dom katikati ya nchi).Dodoma ilipewa status ya makao makuu tangu mwaka 1974 na ikawekwa chini ya CDA.Kwahiyo utaona hapo sababu za kuhamisha makao makuu kutoka jiji la kibiashara kwenda katikati ya nchi zinafanana kote kwa Nigeria na Tanzania ndiomana Nigeria walikuja Dodoma kucopy master plan na kujifunza namna ya uendelezaji makao makuu kutokana na uzoefu wa CDA iliyokua na zaidi ya miaka 16 tangu ianzishwe kwa mudahuo ambao Abuja ilitangazwa kuwa makao makuu.
Na hii ni kawaida sana kwa nchi kwenda kujifunza nchi nyingine kwenye eneo fulani na kucopy idea za huko.....ndiomana hata hapo Rwanda tu jirani wamecopy na kupaste baadhi ya sera za Tanzania kwenye huduma za kijamii n.k
 
upo sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…