Dodoso: Tatizo la Tanzania sio CCM

TAZIZO LIPO KWA WANASIASA KWA KUWADANGANYA WATU KIWA VYAMA VYO NI MWAROBAINI WA MATATIZO.
HALI HII IMEWAFANYA WANANCHI WAWE WAVUMILIVU HATA KWENYE KEJELI HUKU MALI ZAO ZIKILIWA BILA HURUMA.

Vyama na wanaharakati HAWANA mbinu za kuing'oa madarakani CCM na vibaraka Wa Wazungu waliojificha chini ya Chama Tawala na serikali yake .

Wageni ndio wameshika Ardhi KUBWA kuliko wenyeji.

Mo amemilikishwa Ardhi ya nchi Kila Mahali Utafikiri ni mtoto Wa Machafu waliopigania uhuru Wa Nchi hii. KUMBE ALIKUA ni sehemu ya Wakoloni.
Yani Hata familia ya Kinjekitile Ngwale Haina kitu Lakini CCM na WANASIASA walichukua Ardhi ya umma na kuwapa Wageni pamoja na kwamba Ardhi haiozi Wala haihitaji mambo MENGI. Hiví mkonge nao unahitaji teknolojia Gani mpaka apewe mgeni Kwa Malaki ya Ekari Wakati watanzania wengi HAWANA Ardhi Hata ya kujenga.

Bila kutokea shujaa mmoja na kuwafurusha wezi wote na mizizi Yao Ndani ya CCM nchi hii itakua kama Colombia Enzi ya Biashara HARAMU na Siasa za kimafya za wahujumu uchumi.

Lazima atokee MTU aliyeko Mbali zaidi ya Magufuli. Ikiwezekana Hata Makonda apewe nchi awatafune Majizi na kuyatupilia Mbali.
 
Hakika tunapaswa kuji tafakari na kuchukua hatua stahiki kukomesha hii hari.
 
Nimewapuuza sana uongozi wa CDM kuingia kwenye huo utapeli uitwao maridhiano. Yaani utapeli wa wazi wanashindwa kuuona?!
Kweli kabisa, CCM hawapo tayari kwa mapendekezo yote ambayo Chadema wana taka yatekelezwe. 1. Katiba mpya ya wananchi[ hili jambo CCM hawa taki na hawapo tayari na hata katiba itakayo patikana itaendelea kulinda maslahi yao CCM mfano mapendekezo ya kikosi kazi ile yote ndio taswira halisi ya CCM juu ya katiba mpya], 2. Mikutano ya hadhara mpaka leo hii Chadema na vyama vyote vya upinzani vimezuliwa ila CCM wao wana fanya. Yapo mengi tu ambayo CCM wanafanya na kuonesha kuwa taswira nzima ya maridhiano ni usanii mtupu usio na maana yoyote.
 
Nadhan hii imenipa picha kuwa why upinzan hauhangaiki, hawana hamasa tena kama awamu zilizopita, either wamejua, au wameona wanapoteza muda kuipambania jamii isio jitambua
 
Theory yako ndio umefanya tumefika hapa. Tatizo la jamii ya kibongo ikisha zoea hali haibadiliki wala kutaka mabadiliko. Hata wasikie kifu vipi, wataridhika , wameridhika before na wataridhika again
 
Dogo ukome sisi kutuita waoga, Mkoloni tumemzomea tu akaachia nchi. Idd Amini tumempiga mpaka akaenda kuokota taka Uarabun!! Na bado tulikuwa Mstari wa mbele kutetea ndugu zetu wa South

Na kweli walikuwa huru wooote mpaka leo! Zaire Drc mara ngapi tumekwenda huko kuzichapa na waasi?? sasa nakuuliza uoga wetu nini?? nyie ndo baba zenu walikimbia jkt!

Na bado Rais/waziri/katibu mkuu/spika ukituzingua, na kuleta upendeleeo usiyo eleweka tunakunyamazisha kimyaaa! Maisha yako yote! sitaki kuwaambia ni wangapi tumewafanya hivo mnawajua!

sasa mnataka kupigana na mashujaa wa Africa! hebu nikuulize Vyuo vikuu vyooote hivi!! Barabara nzuri, shule matibabu, ma super market ya kufa mtu, zaidi nini?? wewe sema Mungu kakupiga kofi tu bana!
 
Hayo Mapinduzi ni yao hao wazungu! acha kukariri ujinga! siyo unaleta mambo ya kuiga iga tyuuu,,,,,tena ya mwaka 47 hukooo! na sisi tuna yetu ya kisasa na ya aina yake wao ndo wajifunze kwetu! sisi ni waafrica tena wa Brown!

Sie siyo weusi badirikeni!! ndo maana nasema sie ni brown!ya kwetu sisi ni ya kimya kimya tu! hatuui wengi/umati wa waliomo na wasiomo km ya kina Mao!! noo!

sisi yetu ni ya level nyangine tunafinya/nyamazisha Mazimaaa, tena tuna wafanyia wachache wanaojificha kwenye migongo ya maskini walio wengi!! wale wakorofi! siwataji ila mnawajua!

usiombe kunyamazishwa na Dark power ya kibongo, huombi hata maji! na haijulikani Milele yote amina!...wachache sana tunalijua hili! Mwinyi huyo hapo alitenda haki, mzee wa msoga hadi akaitwa dhaifu! wanajua hawa!

hata weye mleta mada usidhani uko mbali hapo! ukituchanganya tu tunakufinya! uone tulivo watamu...kifupi usituletee Yaleee Mapinduzi ya siasa za kishamba ya wazungu! kuuua hovyo bila sababu!

wao wanajutia ujinga walioufanya eti weye waulamba!
 
Hakika mkuu... watanzania bado tupo kwenye usingizi mzito sana, Haki haiombwi duniani pote, tuipambambanie
 
Hakika mkuu... watanzania bado tupo kwenye usingizi mzito sana, Haki haiombwi duniani pote, tuipambambanie
Hakika na hiyo ndiyo sheria kuu ya kudai haki duniani kote “ Haki haiombwi bali haki inapiganiwa”.
 
Hakuna unafuu kwenye dimbwi la umasikini na hatupaswi hata kidogo kujilinganisha na masikini mwenzetu huyo Kenya tunapaswa kuliwazia taifa letu hali ya juu ya kimaisha na sio kuu furahia huu umasikini.
Nani kakwambia sisi ni maskini?,
Uhalisia sisi ni matajiri, tembea ndio utajua ukweli, vinginevyo uhutu na ututsi wenu pelekeni huko huko sisi amani inatutosha,amani tulonayo ni utajiri tosha, msihamasishe wetu kuuwawa ili mfaidike, asipokula huyu atakula yule, hiyo ndio kanuni lazima wawepo wa kula
Bora wale na amani ipo kuliko wasile na vita vishamiri, kama mna hamu ya kupigana nendeni rwanda
 
Wewe jamaa unamakusudi nyingi sana.... kwamba Tanzania kuna amani gani wakati watanzania wengi ni wafungwa wa fikra,
Yaani ni bora ulale njaa kuliko kukosa Amani ya fikra...
 
Ulivyotaja Urusi, Iran ……. Nimeacha kusoma
 
Tatizo bado ni CCM wako tayari kupiga kujeruhi hata kuua ili waendelee kubaki madarakani awamu ya 5 itakumbukwa zaidi kwa kuonyesha rangi halisi ya chama chao.
 
Tatizo bado ni CCM wako tayari kupiga kujeruhi hata kuua ili waendelee kubaki madarakani awamu ya 5 itakumbukwa zaidi kwa kuonyesha rangi halisi ya chama chao.
Hiyo mifano ya nchi zote nilizo orodhesha nazo waliuwawa tena sana kwa hiyo vifo kwenye mageuzi havihepukiki Jambo la msingi mageuzi yetu yawe na msaada kwa Tanzania nzima kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Tuzike kwanza uoga tulio nao ndio kikwazo nambari moja katika kuleta mageuzi katika taifa hili.
 
Mpaka leo hii mwaka 2022 toka uhuru wetu 1961 tumeshindwa kupambana na tatizo letu linalopekea umasikini wetu, ambalo tatizo lenyewe hasa ni “UOGA” hili ndilo tatizo sugu linapopelekea umasikini wetu.
Mkuu nakubaliana nawe kwa 100% bila kufanya hivyo sasa watatuuza kabisa na sisi kwani madalali wa kuuza raslimali zetu wako kazini kwa nguvu zote
 
Historia ya Tanzania kimapambano ndiyo msingi unaoendelea kujibu hali ya sasa. Tulipata uhuru bila mapambano ya kinguvu na hali hii itaendelea hivyo,ila kuhoji kwenye uwajibikaji hilo ni muhimu hata wakati wa kudai uhuru tulihoji kwa majadiliano hilo wananchi walifanye kwa nguvu bila uoga au hofu ni haki yao na wao ndio waajiri wa serikali.
 
Mpaka leo hii mwaka 2022 toka uhuru wetu 1961 tumeshindwa kupambana na tatizo letu linalopekea umasikini wetu, ambalo tatizo lenyewe hasa ni “UOGA” hili ndilo tatizo sugu linapopelekea umasikini wetu.
woga ulijengwa tangu enzi za TAA na TANU na baadaye CCM. Wewe mwenyewe hapo tukikwambia ufanye press usome haya uliyoaandika hapa..... aisee hata kwa mijeredi hutaweza. 🙂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…