Mkuu, kidogo nkukosoe hapo kwenye watu wanaotafsiri literally. Sio wote kabisa. Kwa mfano katika uislam kuna dhehebu moja la kiibadhi (ibadhism) hawa jamaa wana dig deep katika "Quran", wanaitumia quran yenyewe kujitafsiri panapohitajika, wanakuchambulia neno kwa neno. Hebu siku moja usione tabu nenda msikiti wa ibadhi (Ilala au Kitumbini kama upo dar) omba upatiwe mtu mwenye elimu, kisha muulize maswali mawili matatu kuhusu akhera/dunia atakupa elimu, sio lazima usilimu kama hutaki lakini angalau upate elimu, uone kuwa kuna watu wana dig deep katika vitabu takatifu na kuna watu wanachukulia vitu easy easy tu. Tena uzuri wa hawa jamaa ni kuwa sio tu wanatumia hoja za kidini, bali wanatumia akili pia katika kukufanya uelewe jambo. Maana kuna masheikh wengine wao ukiwafuata ukiwaambia mbona jambo fulani hivi, anakukafirisha apo apo, hataki uhoji, lakini hawa maibadhi watakuruhusu kutumia akili yako ili waone umeelewa nini na watatumia akili ili kukuelewesha hoja ya dini ama amri ya dini!