Dogo aliyeonyesha mapenzi kwa mchezaji wa Yanga Donald Ngoma, akabidhiwa jezi

Dogo aliyeonyesha mapenzi kwa mchezaji wa Yanga Donald Ngoma, akabidhiwa jezi

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
dogo1.jpg
Mwandishi wa kituo cha ITV mkoa wa Lindi,Fatuma Maumba, amekabidhi jezi yenye jina la mchezaji wa Timu ya Yanga Donald Ngoma kwa mtoto Juma Bakari,mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Mkwaya,baada ya kukutwa na mwandishi huyo akiwa amevaa fulana lake huku mgongoni akiwa amechora kwa wino wa kalamu jina la mchezaji huyo wa Yanga.

dogo2.jpg


Akikabidhi jezi hiyo kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Newala,Musa Chimaye, ambaye aliona picha ya mtoto huyo kwenye mitandao ya kijamii akiwa amevaa fulana iliyochorwa kwa wino wa kalamu ndipo alipotoa fedha kwa mwandishi huyo ili ikanunuliwe jezi ya mchezaji Donald Ngoma apewe mtoto huyo kwa jinsi alivyoonyesha mapenzi makubwa kwa mchezaji huyo wa timu ya Yanga.

ITV ifikia katika shule ya msingi ya mkwaya,shule ambayo anasoma mtoto Juma Bakari na kukutana na walimu wake na kuelezea juu ya kuwaendeleza watoto wenye vipaji

ITV
 
".....ambaye aliona picha ya mtoto huyo kwenye mitandao ya kijamii akiwa amevaa fulana iliyochorwa kwa wino wa kalamu "

Weka hiyo picha tuione
 
Back
Top Bottom