Dogo anatamani kula madaftari ya notisi.

JEKI

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
4,845
Reaction score
2,957
Ni mdogo wangu, yupo kwenye mitihani, jana nikamkuta na rundo la madaftari na vitabu, analalamika anasoma hayaishi na mtihani ni leo, anasema anasoma akifika mwisho ya mwanzo ameshasahau, basi kwa uchungu akaniambia, ''kaka, natamani kula haya madaftari ya notisi'', si unajua dawa ya moto ni moto, nikamjibu toa photocopy ili uchemshe unywe maji yake kusudi usikose cha kusoma kama utakuta hiyo siyo tiba.

Kusema ukweli dogo ana kichwa kizito, sema kukomaa ndo kunamsaidia.
 
kama ushauri uliompa ndio uliokusaidia na wewe hapo sawa atafanikiwa.
 
yupo level gani ya elimu na fani gani anasoma
 

yupo wodi gadi pale mirembe nimtembelee?
 


[TABLE="class: outer_border, width: 500, align: center"]
[TR]
[TD]kukomaa kumemsaidia ama kumemdumaza?? mbona unatuchachanganyia habari!? aliyekwambia kukomaa ndio kuwa na akili ni nani?

kwa jinsi hali inavyoonesha, mdogo wako hasomi kwa wakati, na wewe kama kaka yake, upo upo tu hata humsaidii mdogo wako kwa wakati pia!

yeye kakuambia suala nyeti sana ambalo wewe ungetakiwa kuwa mshauri wake mzuri wa kitaaluma, mwisho wa siku na wewe unamshauri pumba, mkuu hebu badilika!!!

mpangie ratiba ya masomo mdogo wako, mfuatilie sana juu ya hiyo ratiba kama anaifuatilia na kuitekeleza vile inavyopaswa. mnunulie ama msaidie kupata materials ambazo ziko ndani ya syllabus inayotakiwa na wizara ya elimu, msisitize kusoma sana tena mapema kuliko kusubiri vipindi vya mitihani. huko ni kupaniki tu, hatofanya lolote.

endapo ukifanya hayo, utakuwa kaka bora kabisa katika ujenzi wa familia in micro na taifa in macro!
[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Mwambie akaze msuli elimu sio lelemama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…