The Boss, maswali yako mbona yanajibika tu. Tuchukulie baba hayupo, yawezekana akawa amefariki au walitalikiana au alizaa tu na bwana.
Lengo langu ni kutaka kujua kitakachoenda kichwani mwa mtoto baada ya kupata taararifa hizo au kushuhudia.
Hebu niulize tena, Hivi mwili wamama unahusiana vipi na mtoto? mama si anayo matamanio yake? ina maana hapaswi kujiridhisha atakavyo bali hadi mtoto aamue yupi wa kutembea na mama?
Mimi naamini mama ni binadamu kamili ambaye na yeye anayo mamlaka na mwili wake hata kama akitembea na mwenda wazimu, si ndio mapenzi yake? sasa mimi kama mtoto nitahusikaje kwenye maya mama?
Kwa kuwa jamii imetufundisha kuwa jambo hilo ni baya basi na sisi tunalitafsiri kwa mujibu wa jamii na sio kama sisi.
Tukumbuke kuwa mama naye ni binadamu anayop matamanio yake........ Huo ni mtazamo wangu tu