Kwani si watu wanasoma ili wapate pesa waishi vizuri sasa mtu ukikatizia denge upatikanaji wa pesa shule ya nini? mambo ya mahomuweki mara adhabu sijui umechelewa mara mitihani nani anataka? (Joke.....)
Wasanii wetu wengi wa Kibongo hawajui maisha kwa kweli, na bahati mbaya sana wanashindwa kuona mifano iliyowatangulia. Ni wanamuziki wachache sana waliodumu kwenye fani kwa zaidi ya miaka 6 au 7, wengi huporomoka haraka sana sijui wanakumbwa na nini tu, na ikifikia hapo ndio hukumbuka shule.
Na wanajidanganya sana pale wanapopata shilingi laki 2 au 3 wanaona wamepata pesa nyingi kweli, hizi ni pesa ndogo sana na tena kwa matumizi yao! Lakini nadhani kwao kuwa na jina kubwa kwenye magazeti (especially ya udaku) na kwenye TV ni zaidi ya kuwa na elimu yoyote