Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,506
Msanii wa muziki wa kurap kutoka Tip Top Connection, Dogo Janja amesema anajiandaa kuingia kwenda ndoa siku za usoni kwa kuwa lazima aingie kwenye maisha ya ndoa akiwa na umri mdogo.
Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo Kidebe, amesema kwa sasa hana muda mrefu ataingia kwenye maisha ya ndoa kwani tayari ameshajianda kukabiliana na changamoto za ndoa.
“Hakuna haja yakuogopa, mimi lazima nioe nikiwa na umri mdogo ndo nimepanga hivyo,” alisema.
“Kwanza ni jambo ambalo linampendeza mwenyezi Mungu kwa hiyo hivi karibuni nitafanya hivyo,”
Aliongeza, “Mimi naamini maisha ni haya haya, tena usishangae ukioa mambo yakakunyokea zaidi, kwa hiyo mimi nimesema hivi karibuni nafunga ndoa,”
Rapa huyo amesema Tunda Man aliyefunga ndoa hivi karibuni amemfanya na yeye afikirie kuoa siku za usoni.
Source: Bongo 5