Dogo Janja: Niko mbioni kuoa, ni lazima nioe nikiwa na umri mdogo.

Dogo Janja: Niko mbioni kuoa, ni lazima nioe nikiwa na umri mdogo.

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506
xDogo-Janja.jpg.pagespeed.ic.Aj2FNzGLHP.jpg


Msanii wa muziki wa kurap kutoka Tip Top Connection, Dogo Janja amesema anajiandaa kuingia kwenda ndoa siku za usoni kwa kuwa lazima aingie kwenye maisha ya ndoa akiwa na umri mdogo.

Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo Kidebe, amesema kwa sasa hana muda mrefu ataingia kwenye maisha ya ndoa kwani tayari ameshajianda kukabiliana na changamoto za ndoa.

“Hakuna haja yakuogopa, mimi lazima nioe nikiwa na umri mdogo ndo nimepanga hivyo,” alisema.

“Kwanza ni jambo ambalo linampendeza mwenyezi Mungu kwa hiyo hivi karibuni nitafanya hivyo,”

Aliongeza, “Mimi naamini maisha ni haya haya, tena usishangae ukioa mambo yakakunyokea zaidi, kwa hiyo mimi nimesema hivi karibuni nafunga ndoa,”

Rapa huyo amesema Tunda Man aliyefunga ndoa hivi karibuni amemfanya na yeye afikirie kuoa siku za usoni.

Source: Bongo 5
 
Hasa na wewe muige huyu dogo janja uone maisha yanavokupiga..
 
Cha muhimu umate mate kama upo kuoa lazima hongera dogo janja.
 
Shule vipi?
Shule inataka pesa,ukiwa na pesa hata uzeeni unaenda kusoma,ila familia inatengenezwa wakati bado una nguvu zako,mi namshauri kwa hiyo fani yake ajitahidi kujua kiingilishi.
 
Back
Top Bottom