Doha: Michezo ya Dunia

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,519
Katika wiki hii nimeshuhudia michezo ya riadha, kuruka, kutupa tufe nk. mjini Doha ikifanyika ambapo wanamichezo karibu dunia nzima wako pale. Natumaini na sisi Watanzania tuliwapeleka wana michezo wetu akina Alphonce Simbu.

Tangu michezo hii ianze sijafanikiwa kumwona mwanariadha yeyote kutoka Tanzania. Je akina Simbu wako wapi?.
 
Viwanja vya shule vimeuzwa vyote
Kauli ya PM iwe kweli kama tunataka riadha iendelee
 
Mashindano yanaelekea mwishoni. Hakuna Mtz hata 1
Uganda wana dhahabu 1 kwenye Mbio za 800 kwa Wanawake
 
Mashindano yanaelekea mwishoni. Hakuna Mtz hata 1
Uganda wana dhahabu 1 kwenye Mbio za 800 kwa Wanawake
Sisi watz siasa kila mahali, hatutimizi wajibu wetu!
Hii wizara ya habari utamaduni,sanaa na michezo ni gonjwa SUGU! !
 
Inapendeza... ila hatuna watu wa kupeleka...

Pesa tunafanyia miradi mikubwa...


Cc: mahondaw
 
Uwapeleke Doha unataka wakaumie eee! wataweza kula pizza n sandwiches! wakati huku washazoea kushindia ugali makande 😂 acha hizo kamanda
 
Kumbe kuna wadau wa riadha ! Mimi tangu ianze sibanduki kwenye tv

Leo shock ilikua Michael Norman ambae tulitegema atakua bingwa kumaliza wa mwisho kwenye semi final 400m

Anyway, waTanzania wapo. kwenye marathon ya akina dada siku ya kwanza kabisa alikuepo Failuna Matanga ila hakumaliza.... nadhani kwenye marathon ya wanaume pia watakuepo watatu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…