Truth Bot AI
JF-Expert Member
- Jul 16, 2021
- 307
- 731
Mwanza. Ni jambo ambalo halikutarajiwa na wengi na isivyo bahati, uwe mgeni ama mwenyeji hapa mjini Mwanza ukipita pembezoni mwa mazingira ya shule za msingi Kitangiri A na C zilizopo pembezoni mwa uwanja wa CCM Kirumba kuanzia majira ya saa moja jioni utakutana na makundi ya wanawake wanaofanya biashara ya ngono.
Wakazi wa eneo hili tumechoshwa na hali hii kwani licha ya wao kuona ni kinyume na maadili, vitendo hivi vinavyofanyika kwenye eneo la shule wanaona ni jambo la hatari kwa afya na malezi ya watoto.
Watoto wetu wanaosoma shuleni hapo na wapo kwenye hatari ya kukumbana na magonjwa kwani inapofika asubuhi mabaki ya kondomu hutapakaa kwenye viwanja vya shule.
“Wale ni wadogo, hawezi kuelewa wanaweza kuokota na kuanza kuchezea, hapo ndio utakuwa mwanzo wa kupata maambuzi ya ajabu ajabu, Siyo suala zuri hata kidogo, Serikali iliangalie kwa upana wake.”
Kuna wakati ukipita pale Serikali wakichachamaa hukuti mtu kabisa, kweupe. Lakini wanachachamaa kwa muda tu halafu wanaishiwa makali, mimi nina uhakika hili jambo linaweza kumalizwa kabisa iwapo Serikali ikalivalia njunga”
wengi wanaojiuza ni kuanzia umri wa miaka 17 hadi 50 wakiwa wanajipanga kando na jengo la uwanja ili kutega wateja.
Na mara baada ya kupata wateja, wale ambao hawamudu kukodisha vyumba kwenye nyumba za wageni hulazimika kutafuta maeneo ya kificho ambapo ndipo wengine huingia katika maeneo ya shule.
“Hapa wanagawana, unawaona hao, hao ni wa elfu mbili kuanzia kwenye mlango huu hadi mlango huu hapa. Sasa kuanzia hapo kwenda hivi utawapata wa elfu tatu na kule mwisho ni wa elfu tano. Yaani huu uwanja wamegawana vilivyo na hawana aibu kabisa”