warumi
R I P
- May 6, 2013
- 16,218
- 18,440
Msanii wa filamu na muziki , Ummy Wenceslaus ' Dokii ' ambaye pesa imemtembelea ameonyesha kuwa na ushoga uliopitiliza na msanii mwenzake Lucy Komba baada ya kumzawadia kiwanja kwenye kicheni pati yake iliyofanyika hivi karibuni . Dokii akiwa mmoja wa mastaa waliopamba vyema sherehe hiyo iliyofanyika ndani ya Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa , Posta jijini Dar , wakati wa kutoa zawadi alisema , yeye na Lucy wametoka mbali na ili kudhihirisha walivyoshibana, anampa kiwanja kilichopo maeneo ya Bagamoyo . "Mimi na Lucy tumetoka mbali , tumeshirikiana katika mengi na kudhihirisha upendo wangu kwake namzawadia kiwanja cha eka moja kilichopo Bagamoyo, naamini itakuwa ni kumbukumbu nzuri ya urafiki wetu, " alisema Dokii .