Dokta Amzuia Aunty kujifungulia Marekani

Dokta Amzuia Aunty kujifungulia Marekani

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
DOKTA amempiga stop staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel kwenda kujifungulia nchini Marekani kwa sababu hali yake ya ujauzito aliyofikia haruhusiwi kusafiri kwa kutumia usafiri wa anga kwenda popote.

Chanzo makini kilisema kuwa, Aunt alijiwekea mpango wa kwenda kujifungulia nchini huko kwa muda mrefu lakini alikuwa akisubiri mimba ikue kidogo kitendo ambacho hakikutakiwa kwa kuwa ujauzito umekuwa mkubwa na kusafiri kungemletea tatizo la presha ya kushuka.

“Imebidi nikubaliane na daktari alivyosema kwa kuwa wao wanajua hivyo siwezi kupingana nao naogopa nisije kupata matatizo, bora nijifungulie hapahapa nyumbani na nimelikubali hilo na mawazo ya nyuma nimefuta japokuwa nilikuwa nimeandaa kila kitu kwa safari hiyo,” alisema Aunt alipopigiwa simu.

Awali Aunt alipanga kwenda kujifungulia nchini Afrika Kusini lakini baadaye aliahirisha baada ya kupata shavu kwa marafiki zake waishio nchini Marekani waliomtaka kwenda kujifungulia huko na kukaa kwa miezi mitatu.
 
Marekani ukizaa hata kama wewe auna karatasi mtoto anapewa uraia moja kwa moja ndio maana wanigeria wote kina davido n.k wamezaliwa marekani, Deal hilo kwa future ya mtoto kama mwenzangu na miye

Kwa hiyo jokate nae ana uraia wa marekani?
 
Cheusi dawa nae kwa kupenda makubwa, sasa ukijifungulia marekani ndo mtoto atakuwa mzungu au nfyuuu

Binamu umenichekesha aende Ami hospital masaki wako vizuri nilijifungulia pale atapata huduma nzuri
 
Kwa hiyo jokate nae ana uraia wa marekani?

Ndiyo kazaliwa kule , hata ww binamu kama una pesa yako wife akipata ujauzito unamkimbizia kule akizaa tu mtoto anapewa urahia anapata passport yake unarudi bongo, lolote mbeleni likitokea dogo anatimba zakrle US akasome bure nk....Hao mafisadi wote wake zao na vimada wanazalia marekani sababu ya karatasi
 
Cheusi dawa nae kwa kupenda makubwa, sasa ukijifungulia marekani ndo mtoto atakuwa mzungu au nfyuuu

Hahaha! wanafuata kule ni uraia wa mtoto wake! na ndiyo maana % kubwa ya mastar wa Nigeria wake zao wanaenda kujifungulia marekani!
 
Ndiyo kazaliwa kule , hata ww binamu kama una pesa yako wife akipata ujauzito unamkimbizia kule akizaa tu mtoto anapewa urahia anapata passport yake unarudi bongo, lolote mbeleni likitokea dogo anatimba zakrle US akasome bure nk....Hao mafisadi wote wake zao na vimada wanazalia marekani sababu ya karatasi

Kuna jirani yangu apa mke wake alikuwa ana hamu kweli ya kujifungulia marekani, mpaka akaenda kumbe ndo janja yao? KWa hyo jokate nae mmarekani?
 
Binamu umenichekesha aende Ami hospital masaki wako vizuri nilijifungulia pale atapata huduma nzuri

Tatizo siyo huduma! tatizo anataka mtoto wake awe na uraia wa marekani! hata ukiwa mjamzito ukienda kujifungulia marekan mtoto anapewa uraia wa marekani
 
Hahaha! wanafuata kule ni uraia wa mtoto wake! na ndiyo maana % kubwa ya mastar wa Nigeria wake zao wanaenda kujifungulia marekani!

Hata hao mastar wazazi wao walienda miaka hiyoooo ndio maana wengi wanakaratasi, ni deal ya muda mrefu kwa wanigeria, Nashangaa madada zetu wanaenda kununua nguo za kuvalisha watoto alafu watoto wanazalia bongo kweli akili ni nywele...
 
Huyu hafanyi biashara ya poda kweli? Maisha ya vigodoro yanatosha kwenda marekani kwa ajili ya kujifungua tu au ni gharama ya wanyama wetu.
 
Hahaha! wanafuata kule ni uraia wa mtoto wake! na ndiyo maana % kubwa ya mastar wa Nigeria wake zao wanaenda kujifungulia marekani!

Tena karibia wote ni rahisi na nzuri kitu kikibuma una mpeleka shule za huko huko hadi vyuoni.
 
Back
Top Bottom