Dola Bilioni 1.9 Kuimarisha Gridi ya Taifa Nchini

Dola Bilioni 1.9 Kuimarisha Gridi ya Taifa Nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Waziri wa Nishati, January Makamba amesema kuwa Serikali imetenga fedha kiasi cha Dola za Marekani bilioni 1.9 kwa ajili ya miradi ya kuimarisha gridi ya Taifa kwa kipindi cha miaka minne.

Makamba amesema hayo wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2022/2023 kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Jijini Dodoma.

"Katika Mwaka wa fedha 2022/2023 mradi huu umetengewa sh. Bilioni 500 kwa lengo la kufanya usanifu wa mradi, kupata wakandarasi, kununua vifaa na kuanza utekelezaji wa mradi," amesema Makamba.

Waziri Makamba amefafanua kuwa huu mradi unahusisha ununuzi na ufungaji wa mashine umba 6,000, kusimika nguzo 380,000 za umeme, kununua na kufunga nyaya zenye urefu wa kilomita 46,200 za kusambaza umeme, kununua na kufunga mita za LUKU 700,000.

Amesema fedha hiyo itawezesha kujenga njia za kusafirisha umeme zenye urefu wa kilomita 948 zenye msongo wa kV 132 na kV 22, kujenga vituo 14 vya kupoza umeme wa 220/33 kV na 132/33 kV pamoja na kununua na kufunga mashine umba 66 za ukubwa wa MVA 50, MVA 60, MVA 90 na MVA 120.

Uthamini wa mali za Wananchi watakaopisha ujenzi wa miradi ya umeme imefanyika kwa mradi wa Tabora - Katavi, Tabora - Kigoma, Shinyanga -Simiyu na uthamini unaendelea kwa miradi ya Benako - Kyaka, Songea - Tunduru - Masasi, Kiyungu - Rombo, Kasiga - Lushoto, Mkata - Kilindi, Pugu - Mkuranga na Bunda - Ukerewe.

ikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Athuman Selemani Mbuttuka, wajumbe wa Bodi kutoka taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Nishati, Wakurungezi kutoka taasisi hizo pamoja na watendaji wengine kutoka Wizara na taasisi.

#Nishati
#Miaka2yaSamia
#KaziIendelee
WhatsApp Image 2023-03-25 at 12.35.57.jpeg
WhatsApp Image 2023-03-25 at 12.35.57(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-03-25 at 12.35.58.jpeg
WhatsApp Image 2023-03-25 at 12.35.58(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-03-25 at 12.35.58(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-03-25 at 12.35.59.jpeg
 
Nifunze kuweka picha vizuri.

Harafu sema zaidi ya sh.Tilioni 4 kuimarisha Gridi.

Mwisho hayo yaliyotajwa huko yakifanyika basi mambo yatakuwa mazuri.
 
Back
Top Bottom