Dola ikifumba macho CCM inasambaratika

Dola ikifumba macho CCM inasambaratika

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Natabiri kifo Cha CCM kitatokana na dola kutumba macho. Chama Cha siasa kisichokuwa na wanasiasa kimekufa. CCM inakimbia kwa kasi ya ajabu sana kuikumbatia dola na kuachana kabisa na siasa.

Hakuna chama Cha siasa kinachokuzwa na dola, dola inalinda tu kwa kuzingatia matakwa ya amri za mara kwa mara. Ikitokea dola ikakosa mtu wakuiamrisha uwezi kuiona ikiangaika na siasa ya chama chochote, inakaa kimya.

Nape alikuwa mwana ccm na alikua chini ya dola, dola ilipoambiwa huyu tumemtema walishughulika naye kisawasawa. Malima alikuwa Mbunge na Waziri, Masha, Membe, Lowasa, Sumaye nk walikuwa wanakomand dola ila dola ilipoambiwa acha kumtii huyu waliacha wakaanza kushughulika nao.

Nimetoa mifano hii kuwakumbusha ccm kwamba wapo kwa sababu dola inaelekezwa kuwafanya wawepo, siku dola ikisinzia kwa dakika chache basi wanapisha.

Njia pekee ya CCM kujiaminisha kuwepo ni kuchanganya nguvu ya dola na nguvu ya umma. Dola ikikukataa umma unakuunga mkono so unabaki kuwa na nguvu kwa sababu umma ndio unaowasimamia dola. CCm inapochimbia mizizi kwenye dola inajichimbia mizizi ya kuanguka.

Nape alipotengwa, dola ikamkataa faraja yake ilikuwa ni umma wa Watanzania na Wana Mtama. Alipowadharau wana Mtama akakataa kura zao kupitia sanduku la kura tarehe 28/10/2020 na kuegemea kwenye dola ile nguvu ya umma iliachana naye bila yeye kujua.

Nini umma unacho ambacho dola haina ndicho kinachofanya mwanasiasa kujitafakari anapoamua kufanya siasa. CHadema na ACT hawana dola ila Wana umma nyuma yao, kila dola inapotaka kupambana nao umma unanyanyuka nakuwatetea katika kila Kona Jambo linalowafanya walioshika dola kutumia nguvu kupambana na umma badala ya kujichanganya na umma kuwapunguza nguvu Chadema na ACT.

Nguvu ya umma ni kubwa, viti maalumu kumi na tisa wa Chadema Leo wakihitisha mkutano wa hadhara hakuna mwananchi atakayewasikiliza kwa sababu wao wameambatana na dola wakajiona niwakubwa kuliko umma.

Bila dola kuwa nyuma yao hakuna siasa ndani yao hadi pale watakaporudi kwa umma kuomba kuungana na umma kuusaidia umma kupunguza kasi ya dola ambalo ni waajiriwa wa umma.

Ni Jambo gumu ila ukweli ni kwamba dola haina rafiki wa kudumu wa adui wakudumu, umma una rafiki wa kudumu na adui wakumu....jitengenezeni kuwa marafiki wa umma kujiandaa na makabiliano na mashinikizo ya dolla.

Leo hii mbunge aliyekua na uwezo wa kuchaguliwa kwa asilimia 70 na umma hakuchaguliwa na umma Bali alipitishwa na dola. Madhara yake ni kwamba mbunge huyo ni mtumwa wa dola Hadi amalize muda wake. " Kama siyo mm usingeupata huo Ubunge"

Tujitafakari
 
Unaongea hisia zako hujui lolote. Kama hujui ushirikiano wa dola na CCM ukoje bora ukakaa kimya. Unajua asilimia 98(98%) ya TISS ni CCM?... Unajua kwa nini system imesetiwa hivyo!? Mambo mengine achana nayo, yamekuzidi kimo.
 
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imeanzishwa na CCM

Vyama vyote unavyovijua wewe Tanzania mpaka usiku huu katika top ten ya viongozi wake wa juu atleast mmoja ni mtuu wa 'CCM'

Pale Chadema katika viongozi wa juu kabisa top 5 yupo mtu mmoja wa CCM

Dola na Ccm ni kama Bahari na chumvi yaani Lila na Fila hazitengamani

Dola inaitegemea Ccm na ccm inaitegemea Dola
 
Unaota kwa sasa ,labda baadaye .Ndoto yako inaweza kuwa ya kweli au sio.Mwenyekiti wa chama ndio Rais wa nchi .Miaka kumi kwa CCM ni mfumo tofauti wakutuongoza dola
 
Dah!! una akili sana wewe mtu. Sijui kama hawa watu watakuelewa.
 
Unaongea hisia zako hujui lolote. Kama hujui ushirikiano wa dola na CCM ukoje bora ukakaa kimya. Unajua asilimia 98(98%) ya TISS ni CCM?... Unajua kwa nini system imesetiwa hivyo!?... Mambo mengine achana nayo, yamekuzidi kimo.
Kumbe unakiri kuwa CCM inabebwa na TISS?
Kwa hiyo TISS ibadilishwe jina iitwe USALAMA WA CCM sio wa Taifa tena.
 
Ndoto unayoota inachekesha sana 😂😂😂
 
Back
Top Bottom