Dola ya kale ya Kiislam (Mesopotamia) ilitawala Dunia Takribani miaka 500 na ilikuwa sana, ila ilikuwa na tatizo kubwa moja

Dola ya kale ya Kiislam (Mesopotamia) ilitawala Dunia Takribani miaka 500 na ilikuwa sana, ila ilikuwa na tatizo kubwa moja

smaki

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2019
Posts
4,976
Reaction score
3,098
Ndg km ilivo kivhwa cha nabari kwanini hii Dola Mesopotamia yenye nguvu kiuchumi, kijeshi, hivo, ilikuwa haina mpango wa kutwaa nchi za Africa kama sehemu ya Colon lake?

Sifa kubwa ya Waarabu ni waliijua vyema Africa kuliko Wazungu walivo dhani, licha ya kuzunguka miaka 400 Barani humu wakifanya Biashara ya Utumwa, na Pembe? Walijua Dola zipi za kienyeji zilikuwa hazishikiki.

Kinyume na Dola ya Kiislamu kutwaa Bara tajiri sana Duniani, kuanzia watu na vyote vilivyomo! zilikuja nchi za Ulaya zikagawana kiulaini kabisa, wakajikatia mapande as if hakukuwa na watu Barani Africa!

Kumbuka wakati wa kuligawa Africa, hapa kwetu Tanganyika kulikuwa na jumla ya watu laki nne tu (400,000) population wise! nchi km the United KIngdom of the Great Britain, Ufaransa, nk

Hawa walikuwa ni nchi maskini, sometimes kuliko Africa, waliwezaje kuingilia waarabu sehemu yao ya biashara bila kupingwa? Africa tena kiulaini kabisa.

Mpaka leo Ulaya inatawala Africa yote Kisiasa tokea Cairo mpaka Cape town! Mfaransa, na M-U/Kingdom, hawaingiliani, na wameshika Makoloni yao ni si kitoto!

Hili Dola la kiislamu je walikuwa vilaza kiasi kwamba hawakuona fursa, ya Madini na ardhi nzuri? au walipigwa kauzibe?

Je, kule Berlin conference sikuwahi kuona Taifa mojawapo la kiarabu lilioalikwa kuhudhuria! kwa nini? Urusi, Japan, China zilikuwa na nguvu kwa nini hazikualikwa?

Je, tunaweza kupinga maamuzi Batili yaliyotolewa kwenye mkutano ambao hata wawakilishi kutoka Africa hawakuwepo? Maamuzi ambayo mpaka leo yanatuathiri nchi zote za AFRICA kisiasa.

Kwa nini wa-Africa tusiwagomee Weupe? Hakuna kwenda, kula wala kununua kwao! Tupige kimya tu! naamini NGOs, AU, SADDC, ECOWAS nk zote zikiamua kuhamasisha inawezekana!
 
Kwanza nafikili ile berlin conference ndo imetufikisha hapa tulipo. Lengo la kile kikao ilikua ni kumfanya mwafrika awe mtumwa wa milele .matatizo tunayopata waafrika yote ni matunda ya kile kikao.
Utetezi wako ni mtu anayekwepa uwajibikaji wa maisha yake
 
Mwislam hajawahi kuitawala dunia
Opera Snapshot_2020-04-19_053017_www.aljazeera.com.png
Tena alikuwa mshindi kweli kweli vita, Pande za Ulaya ya Kusini, akazibidilsha nchi za ukanda huo kufuata imani za kiislam, akafanikiwa, ngoma ilikuwa nzito alipofika Rome! rejea During Islamic Golden age!
 
Hii Corona inaweza kutugawa nao na kutuonesha bila wao tunaweza tatizo litakuja kwa wale wazee wa scholarships na wanasiasa Kwan CC wenyewe ndio hua tunajikaanga tukiiva watu wanakuja kula gadaf kufa ilitukost Sana waafrica Kwan bila ivyo Africa ingekua imesha eleweka

Sent using Jamii Forums mobile app
Mzalendo .umeongea ukweli kabisa alafu wale viongozi wa kiafrika walio jitahidi kuleta maendeleo waliuawa au kupinduliwa
 
Dunia gani unayoimaanisha ukisema ancient Mesopotamia iliitawala. Kwanza hata Afrika yenyewe haikutawaliwa na Mesopotamia, walijihusisha na Egypt uko na wala sijawahi soma popote kuwa waliitawala. Dola ambazo zilijaribu kutwaa maeneo makubwa duniani ni Warumi na wavamizi wa Mongolia kina Genghis Khan na mjukuu wake Hulagu Khan.

Huyu Britain alijitahidi kuitawala dunia kwa faida in modern times na si kwamba alishindwa kuwa na eneo kubwa, bali aliona hana sababu ya kuwa na maeneo mengi ambayo hayana faida. Hata wakoloni wengi walifanya hivyo ndo maana Ufaransa alitoka akaenda mbali kuchukua Indochina. Ndo maana Britain aliacha nchi kibao akaitwaa Australia na kukomaa nayo. Na pia kulikuwepo upinzani wa mabeberu wenzake.
Spain walikuwa wana makoloni yenye mali nyingi lakini kwa vile walikuwa wazembe wakapoteza nafasi na wako wa kawaida hadi leo.

Huyo Otto von Bismarck aliita mjadala wa kuepusha mapigano wakati wa kugawana makoloni. Muda huo ilikuwa miaka michache ametoka kuiunganisha Ujerumani, yeye nadhani alitokea jimbo la Bavaria. Aliunganisha vijimbo vingine akatengeneza Ujerumani na ndo maana akaitwa Chancellor wala sio mfalme.

Warusi wasingeitwa kuigawa Afrika kwa vile hawakuwa na nia hiyo, wao wana eneo kubwa wanashindwa kulitumia then waende kuchukua eneo lingine tena.
 
Hata Roman empire haikutawala dunia na walimenyana Sana na wafaransa,Mongolia hakufika hata ulaya,british empire walijitahidi kidogo kufika Hadi Africa wakimenyana na wajerumani na pia wafaransa,
Otoman empire alitawala Asia na sehemu za Europe,akakwama romani empire,hakunaga dola ilitawala dunia nzima
 
Swali wakati wazungu wanakuja kuitawala Africa, wao walikuwa na maendeleo gani kiuchumi?

Maendeleo Kisiasa nadhani hawa wakoloni kuwa chini ya uongozi wa kifalme ilikuwa ni uongozi imara thus why wakafanya maamuzi ya kibabe kuitawala Africa.

Sent using Fly in any Weather.
Wazungu walikuwa washakuwa organized. Mfano Waingereza walikuwa washamalizana na 100 years of War na Ufaransa. Walikuwa washapitia kipindi cha War of Roses. Walishatawaliwa na Vikings kutoka Kaskazini maeneo ya Sweden. Walishapitia kipindi cha kuwa na noble family na knights. Washatawaliwa na Habsburg family ambao asili yao ni Spain.

Walikuwa washapita vipindi vya kipuuzi vyote ndo wakasettle then badae wakaja na Industrial revolution miaka ya 1700 uko. Wakawa na uzalishaji viwandani, wakagundua nchi yao ina rasilimali chache sana. Wakawa na shauku ya kuendelea zaidi.
Sayansi na teknolojia ikakua kwa vile kwanza wako na amani hivyo wana muda wa kutumia kwenye innovation za civilian use. Wakaunda navy imara.

Navy ikawasaidia kulinda visiwa vyao na njia za bishara karibu yao, maeneo kama Giblaltar. Wakadhamini wapelelezi, wakadhamini hata maharamia (maharamia walianzia Uingereza na ufalme wa nchi hiyo ulikuwa unawaruhusu ilimradi wanagawana faida ya mali zilizoibiwa).

Walikuwa wanaijua Misri. Misri haikuitwa Afrika kwa vile Suez canal ilikuwa haijachimbwa hivyo ngamia za waarabu zilitoka kwao na kuingia Misri kwa nchi kavu. Wareno wakataka kutafuta route nyingine ya kufika far East kwa lengo la biashara, wakamtuma Vasco da Gama na wenzake. Wakati huo na Spain iko mbioni.

Baadae Afrika ikajulikana na mashirika yakatuma watu waje kufanya research uku, kina Livingstone, (Steamer?) na Speke. Serikali za wazungu zilipopata taarifa hizo zikaja mbio kutwaa maeneo kwa faida zao. Wazungu wote advanced wakajua kinachoendelea, ndo tunarejea Berlin.
 
Maelezo mazuri mkuu , umeelezea vizur ilikuaje before, Hadi badae ikafikia hatua ya Berlin conference

,hakunaga dola ilitawala dunia nzima
Mkuu Elungata niliwahi soma pahala panasema wakati huo! watu walikuwa siyo wengi sana kama ilivo kuwa miaka ya baadaye kidogo! population kubwa ilikuwa Africa kaskazini, Middle East ya leo kwenda mpaka India,hapo ndo ilikuwa Dunia

Ulaya yote ilifunikwa na Barafu, Gracial age in Europe, iltokea polepole Neanderthal -wazungu wakahamia kule na kuzaliana

kwa sababu ya matumizi mabaya ya ardhi na kukata Miti hovyo kulipelekea kutokea jangwa la Sahara, which means hapo palikuwa ni pa kijani, huku kusini mwa Ikweta ilikuwa ni Wanyama wakali tu na watu wa kabila la Wabarbaig/ Khoisan.

kwa mfano leo Bara Antarctica hakuna watu, inawezekana miaka 200 ijayo watu wakaishi. hili unalisemeaje kimfano?
 
Shukrani Kwa ufahamu mzuri nimeelewa vizuri sana. Kwahiyo Africa kwa sasa hatuwezi kupita njia hizo tukafanikiwa kimaendeleo.

Ili tufanimiwe inatulazimu kwenda sawa na wazungu walipofika sasa?:-

1. Kiubunifu
2. Kiusimamizi
3. Kiuzalishaji
4. Kimasoko

Je tukikata mahusiano na nchi za ulaya kisiasa, kiuchumi na kimaendeleo tukakomaa Africa kama Africa kushirikiana katika uzalishaji na kuuziana bidhaa tutatoboa?

Sent using Fly in any Weather.
Shukrani mkuu.

Huwezi kupata maendeleo kwa kujitenga na wazungu. Wao wameturahisishia njia za kufika mafanikio. Wao wametupatia theory na practical ni kazi yetu. Huwezi anza kudhamini ugunduzi wa gari sasahivi, utapoteza muda. Chukua model moja Ulaya uko, fanya reverse engineering utapata pa kuanzia kuliko kuanza kazi za Karl Benz alizofanya miaka ya 1800s mwishoni.

Nchi zote zilizoendelea baada ya kutawaliwa zimewakumbatia wazungu. Vietnam, South Korea, Republic of China, Singapore, Peoples Republic of China,. Hata kwetu Afrika; South Africa, Egypt, Morroco na Algeria wako wanavuna manufaa ya kukaa karibu na wazungu.

Ukikaa karibu na watoto wa kishua unafaidika kuliko kukaa na maskini mkashauliana uchawi.
Achana na mawazo ya hawa walitutawala. Unataka Canada waseme nini, Australia waseme nini, Hong Kong waseme nini. Wote hao walikuwa na bado wana element za Mwingereza.
 
Mkuu Elungata niliwahi soma pahala panasema wakati huo! watu walikuwa siyo wengi sana kama ilivo kuwa miaka ya baadaye kidogo! population kubwa ilikuwa Africa kaskazini, Middle East ya leo kwenda mpaka India,hapo ndo ilikuwa Dunia

Ulaya yote ilifunikwa na Barafu, Gracial age in Europe, iltokea polepole Neanderthal -wazungu wakahamia kule na kuzaliana

kwa sababu ya matumizi mabaya ya ardhi na kukata Miti hovyo kulipelekea kutokea jangwa la Sahara, which means hapo palikuwa ni pa kijani, huku kusini mwa Ikweta ilikuwa ni Wanyama wakali tu na watu wa kabila la Wabarbaig/ Khoisan.

kwa mfano leo Bara Antarctica hakuna watu, inawezekana miaka 200 ijayo watu wakaishi. hili unalisemeaje kimfano?
Unaijua Camerot iliyokuwepo kule Scotland miaka ya kabla ya Yesu. Unaijua Ujerumani (ambayo haikuwepo kipindi hicho) ambayo watu wake waliitwa Barbaric tribes na Warumi kipindi wanaitawala.
Hivyo kusema glaciation ilikuwa haijatokea unakosea sana kwenye geography ya dunia. Ilikuwa ishatokea maelfu ya miaka mingi yaliyopita. Sema tu watu wa maeneo hayo hawakuwa na influence na walikuwa disorganized.
 
Back
Top Bottom