Comred Mbwana Allyamtu
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 351
- 887
UFALME WA KONGO: "WENE WA KONGO, FALME PEKEE AFRIKA ILIYOKUWA YA KWANZA KUWA NA DEMOKRASIA NA DIPLOMASIA.
Na. Comred Mbwana Allyamtu (CMCA)
Thursday- 9/06/2022
Marangu, Kilimanjaro, Tanzania
Ufalme wa Kongo ambao ulijulikana kama "Wene wa Kongo au Kongo dya Ntotila" ni mojawapo ya falme za Kiafrika za kale zaidi na zilizoandikwa vizuri, Wanahistoria wanaeleza kwamba ufalme huo ulihusisha sehemu za Angola ya leo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na Jamhuri ya Kongo ya sasa.
Hata hivyo, hadithi iliyosimuliwa na wenyeji inadai kuwa dola hiyo ilienea pia sehemu za Gabon ya sasa, Namibia na hata Zambia.
Kufanana kwa tamaduni za eneo hilo zinafanya kuunga mkono hoja hii, japo kuna upungufu wa ushahidi wa kutosha kuthibitisha hilo kwa baadhi ya sehemu.
Hata hivyo.....
Historia ya ufalme huo inaonyesha maendeleo makubwa ya Afrika katika ustaarabu, maendeleo na muundo wa kisiasa, kijeshi, kiteknolojia na kiuchumi wa ufalme huu wa Kiafrika, kabla ya ujio wa wazungu na wageni wengine kutoka nje ya Afrika.
Ushahidi unaonesha kuwa ufalme huu wa Kongo ulianzishwa na mfalme wa kwanza aliyeitwa Nimi the Lukeni, ambae anayejulikana pia kama "Lukeni Moon Nimi" mwaka 1390.
Huyu Lukeni Moon Nimi alikuwa mtoto wa Nimi a Nzima kutoka eneo la jimbo la Base Kongo ya sasa kule Jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo (DRC), mama yake alikuwa ni Lukeni lua Nsanze.
Ufalme wa Kongo ulianza bonde la mto Kwilu (Kwilu River), Mfalme Lukeni Moon Nimi aliendesha uvamizi na kuteka eneo la Mbanza, na kumfurusha mtawala wa eneo hilo aliyeiywa Mwene Kabunga au Mwene Mpangala na kujenga ngome yake hapo, baadae hapo pakawa mji wake mkuu.
Mfalme Lukeni Moon Nimi akajipa cheo cha Ntinu na kuanzisha ufalme wake wa kongo hapo, aliuita ufalme wake jina la Kongo kufatia asili ya kwao huko Bakongo eneo ambalo mto kongo unamwaga maji yake kwenye bahari ya Atlantic.
Neno Bakongo linamaanisha watu wa kongo yani watu wa eneo la mto kongo, hivyo aliita ufalme wake kurejelea jina la asili ya alikotokea.
Lukeni Moon Nimi anachukuliwa kuwa ndio mwanzilishi wa Ufalme wa Kongo, ingawa wengine wanauhusisha uanzilishi wa falme hiyo na baba yake Nimi a Nzima.
Lukeni Moon Nimi alikufa akiwa bado kijana, mwanae Nkuwu a Ntinu, hakuruhusiwa kumrithi, moja ya sababu zinazotajwa kushindwa kumrithi ni kutokana na sababu za kijadi, cheo cha ufalme kilienda kwa binamu ya Lukeni aliyeitwa Nanga wa Kongo, Lukeni Moon Nimi alifariki mwaka 1427.
Ufalme huo ulieenea eneo lote la Afrika ya kati kupitia uvamizi na kupokea wahamiaji kadhaa kutoka kusini na kaskazini mwa Afrika kuanzia karne ya 12 hadi 15.
Inatajwa kuwa ufalme wa Kongo ulikua na mtandao mkubwa wa kibiashara, Ufalme huo uliyeyusha shaba na dhahabu na kuzifanya bidhaa katika biashara ya mabadilishano na bidhaa zingine kama vile nguo na bidhaa za ufinyanzi.
Karne ya 15 ufalme huo ulikuwa ndio kitovu cha njia za biashara za pembe za ndovu, shaba, nguo na vyombo vya ufinyanzi, katika ukanda wote wa Afrika ya kati.
Wafanya biashara kutoka Afrika mashariki, magharibi na kusini walipita Kongo kama njia kuu na salama kwenda ukanda mwingine kibiashara, dola ya Kongo ilikusanya ushuru wa vitu kama ngombe, chakula kama tozo ya ushuru kuruhusu wafanya biashara kupita.
Mji mkuu wa ufalme wa Kongo ulikuwa ukiitwa Mbanza Kongo, huu mji wa Mbanza Kongo, kwasasa mji huo upo nchi ya Angola katika jimbo la Zaire, mji huu ilianzishwa mwaka 1390, na awali uliwahi kuitwa Nkumba a Ngudi pia ukaitwa Mongo wa Kaila na mwisho ukaitwa Kongo dia Ngunga kabla kuitwa tena Mbanza Kongo.
Mji wa Mbanza Kongo ulipata umaarufu kiasi kwamba ujio wa Wareno wa kwanza mwaka 1483 waliupa jina la São Salvador.
Wareno walipokelewa hapo na kuishi kwa miaka mingi, waliwabadili dini viongozi na wakaazi wa falme hiyo na kuwafanya wakristo.
Ufalme huo ulikuwa na utawala wa mikoa ambapo kila mkoa wa ufalme huo ulikuwa na mji mkuu wake, ufalme wa Kongo unachukuliwa kama ndio dola pekee ya kale Afrika iliyokuwa na serikali ya muungano na ya kidemokrasia kwa Afrika.
Mfumo wa elimu katika falme ya Kongo yani Bakongo (watu wa ufalme wa Kongo) walijifunza kilimo, uwindaji na ufugaji pia walijifunza biashara kupitia elimu maalumu kutoka kwa walimu na wasomi wa falme hiyo.
Pia dola ilijenga shule za kifahari nyingi katika meneo ya mji mkuu na sehemu kadhaa za ufalme, kati ya hizo maarufu zaidi ni pamoja na shule ya Kimpasi, Kinkimba, Buelo na Lemba, shule hizi zilibuniwa kutoka kwa wasomi wa ufalme huo, ambao baadhi yao walipelekwa Ureno kujifunza utamaduni na Maarifa mapya.
Katika UCHUMI, falme hiyo ilianzisha Fedha yake ambayo iliyokuwa ni ganda la konokono wadogo wa baharini, fedha hiyo iliitwa "Nzimbu".
Nzimbu mia ingeweza kununua kuku 300, jembe la bustani na mbuzi 2000, Magamba ya Nzimbu yalikusanywa katika kisiwa cha Luanda na kuwekwa au kutunzwa kama hazina ya ufalme.
Magamba ya kunokono yaliyoitwa nzimbu ndio yaliruhusiwa kufanya biashara kwa mabadirishano ya bidhaa, Nzimbu 200 zingeweza kununua dhahabu au fedha 500.
Katika ufalme wa Kongo wanawake katika majimbo mbalimbali ya ufalme wa Kongo waliweza kutekeleza majukumu ya uongozi na hata kuwa askali ambao waliruhusiwa pia kwenda vitani.
Katika Ufalme wa kongo kulikuwa na mfumo wa kipekee wa kiutawala na kisiasa, mfalme ambaye alitawala alisaidiwa na baraza la washauri 10 wenye busara walioteuliwa na mfalme kuunda mahakama ya kifalme ambao wao walikuwa wajumbe maisha yao yote.
Pia mfalme wa ufalme wa Kongo alichaguliwa na baraza la wazee na wajumbe kutoka kila jimbo, katika miji yote ya Ufalme kulikuwa na wajumbe ambao pia walichaguliwa na raia wa falme ya kongo, kila kitu kilifanyika kwa msingi wa ridhaa ya pamoja, ambayo inafananishwa na demokrasia ya sasa.
Kwenye ufalme huo mfalme aliweza kuenguliwa na wajumbe (baraza la ushauri na nidhamu la Mahakama ya kifalme) ambayo iliiundwa na wajumbee wazee 10 wenye busara, sababu zilizoweza kufanya mfalme awezekuenguliwa ni pamoja na kosa la utovu wa nidhamu au kushindwa kuwaongoza wananchi.
Mfalme alitakiwa kuhakikisha usawa kati ya waBakongo wote katika himaya yake, alitakiwa pia kudumisha utulivu wa kinidhamu katika jamii yake, na aliwasaidia wanajamii kuishi kwa unyenyekevu.
Mfalme aliheshimiwa na kuwakilishwa katika majimbo na magavana ambao aliwateua kutumikia kwa miaka 3.
Katika dola ya Kongo Ufalme haukuwa wa urithi, hii ilimanisha kuwa kwamba raia yeyote wa ufalme wa Kongo yaani Mkongo yeyote yule angeweza kuchaguliwa kuwa mfalme.
Kiti cha ufalme kilibaki wazi ikiwa mfalme aliyopo atavuliwa ufalme, kufariki dunia au kujiuzuru, ikiwa hayo yatatokea basi uchaguzi unafanyika kumtafuta mfalme mpya.
Mchakato wa uchaguzi usimamiwa na baraza la watu kumi ambalo ndio huitisha uchaguzi na kuusimamia, mtu yotote aliruhusiwa kugombea kwa kuanza kupigiwa kura kwenye mjimbo na kisha kupata wagaombea 10 baada ya mchujo.
Hawa wagombea 10 ndio upigiwa kura kwenye baraza la wajumbe kutoka kila jimbo, Ufalme huo ulikuwa na majimbo 10, yakiongozwa na magavana 10 ambao nao waliteuliwa na mfalme.
Majimbo hayo yalikuwa ni Soyo, Ngoyo, Kakono, Loango, Mpumbu, Nsundi, Mbamba, Mpemba, Mpangu na Mbata.
Mfalme wa Kongo alikuwa na cheo ambacho rasmi kilijulikana kama "Mwenekongo" (Mfalme wa Kongo), na watawala wa majimbo mengine, walishikilia vyeo vyao vya uongozi wa kila mkoa vikiambatana na kiambishi awali cha "Mwene", kwa mfano, kiongozi wa jimbo la Mpangu alikuwa akiitwa "Mwene Mpangu", na yule wa jimbo la Nsudi alikuwa akiitwa "Mwene Nsudi".
Pia mfalme aliteua watu 3 ambao wao walipewa kazi ya kuzalisha mawazo mapya ya kisiasa au falsafa ambazo zingesaidia kuongoza Ufalme.
Baraza la kutunga sheria la ufalme wa kongo liliitwa "Ne Mbanda-Mbanda" ambalo kila jimbo lilitoa mjumbe mmoja kwenda kujadili masuala ya dola hiyo na kupitisha sheria ya ufalme huo.
Bakongo (watu kutoka Ufalme wa Kongo) waliunda mfumo ambao ulifanya kazi kwao na kuzingatia utamaduni na maadili yao.
Mfumo wao wa kumchagua mfalme wa Kongo na wasaidizi wake hakika haukutokana na mfumo wa kidemokrasia wa Kigiriki (Democratia).
Kutoka mwaka 1390 hadi 1862 ufalme huo ulikuwa ni dola huru, lakini Kuanzia mwaka 1862 hadi mwaka 1914 ufalme huo ulikuwa kama jimbo la kimila lisilo na mamlaka kamili chini ya Ufalme wa Ureno ambayo kipindi hicho Ureno ndio alikuwa mkoloni wa nchi ya Angola.
Kugawanywa kwa bara la Afrika mwaka 1885 mikononi mwa wakoloni wa kibeberu pia kulifanya ufalme huo kugawanyika mikononi mwa wakoloni wa kizungu, sehemu kadhaa ilibaki Angola, nyingine ikaenda Kongo Kinshasa, Kongo Brazzaville, Zambia na Gabon.
Mfalme wa mwisho alikuwa ni
Mfalme Manuel III ambae alitawala kuanzia mwaka 1911 mpaka mwaka 1914.
Mnamo mwaka 1914, kufuatia uasi wa Ufalme wa Kongo kwa serikali ya Wareno, serikali ya Ureno iliufuta na kuupiga marufuku utawala wa kifalme eneo hilo la falme ya kongo.
Cheo cha mfalme wa Kongo kilirejeshwa tena mwaka 1915 baada ya mfalme Manuel kuomba msamaha na kukubali kuwa kibaraka wa Ureno hadi mwaka 1975, kama cheo cha heshima bila mamlaka halisi.
Maeneo ya ile iliyokuwa ufalme wa Kongo zamani katika nchi za Angola, Kongo ya Kinshasa, Kongo ya Brazzaville na eneo la Cabinda kwa sasa yana kundi la kisiasa linaloitwa "Bundu dia Kongo" ambalo linataka kufufua ufalme na kujitenga kutoka Angola, Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Gabon ili kuunda dola ya Kongo tena.
Hii ndio dola ya ufalme wa Kongo ilio kuwa na maendeleo makubwa ya demokrasia kuliko hata mataifa ya Ulaya, kipindi hicho cha miaka ya 1300-1700 nchi nyingi za Ulaya zilikuwa bado zipo kwenye changamoto nyingi za kiutawala, kiuchumi na ububusa mwingi.
Hii ndio Kongo kingdom (ufalme wa Kongo) ambayo ulaya ilijifunza kwetu ustaarbu na ustawi.
Hii ndio Kingdom of Kongo au "Wene wa Kongo au Kongo dya Ntotila" dola pekee ya kale Afrika iliyokuwa ya kwanza kuwa na serikali ya muungano na ya kidemokrasia kabla wazungu awajatugeuza kuwa Mende.
📌 Kwa kupata makala Zaidi wasiliana na Mimi WhatsApp 0679555526 uungwe group la Maktaba Kuu kwa gharama ya Tsh 3000/=.
👉📎 Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
®Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu.
Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
© Copyrights of this article reserved
®written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika Kwa mawasliano
™Comred Mbwana Allyamtu
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com
© Copyright 2022, All Rights Reserved.
📎Maktaba Kuu.