Dola ya wachaga kabla ya uhuru

Mangi alikosea sana. Alitakiwa akomae Chagaland iwe nchi huru. Hakukuwa na sababu ya kujiunga na Jamhuri ya Wadanganyika
 
Asante kwa historia nzuri. Picha mbona hujaonyesha ya hao ma mangi? Kuna utafiti mmoja unaelezea koo za wachagga nilikuwa nao in pdf nikapoteza nikifanikiwa kuupata nitauleta hapa.
 
Duh kwakweli wachaga wapo smart tangu zamani sijui ni kwann watu Wana chuki na watu Hawa
kumbe maendeleo tunayoyaona uchagani yaliasisiwa kitambo
mangi mareale alikuwa moja ya watz 2 kuwa na Masters ya uchumi kabla ya Uhuru,pia walikuwepo wasomi kadhaa include Dr kleruu,nsilo swai etc
jeshini ndio usiseme Vita ya kagera waliokuwa viongoz wa vikosi wengi walikuwa Chagas na pares
example mej jenerali tumainiel kiwelu,Imran kombe, Kimario,brigedia general Benjamin msuya etc
Mungu aendelee kuibariki Kilimanjaro
britanicca
Come27
tinkanyarwele
instanbul
Sky Eclat
Rweye
Frank Wanjiru
chuma cha mjerumani
Otorong'ong'o
Upepo wa Pesa
sikongefdc
last king of uscoch
MBIIRWA
 
Ingawa sisi ni makabila mengine tukubaki tu kwamba wachagga wametutangulia; tuna mengi sana ya kujifunza toka kwao.

Mfano mdogo tu miaka ya 80 wao walikuwa na Sec karibu kila kata tayari, tena zenye ubora wakati huo huku kwingine yalikuwa majanga matupu.
 
Najuwa wenye chuki watakosoa kwa hila zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanamaliziamalizia kunywa mbege kabla ya kuanza safari ya kutoka Moshi.

Huu uzi umeanzia whatsapp, ni katika kuendeleza ile spirit ya nyumbani ndio maana wanakumbushana historia.

Sio ajabu mwakani tarehe kama hizi huu uzi ukasambazwa tena.
 
Muandishi na mleta mada naona wote aidha hawana ufahamu wa kutosha wa uongozi na historia ya uongozi ambao ulikuwa na ufanisi na ushawishi ili matakwa yake yakue.

Kama kweli wachaga wangekuwa na nguvu thabiti ya uongozi, basi ilitakiwa wakuze dola yao kutoka mkoa mmoja wa Kilimanjrao na kuleta ushawishi wa utawala wao mikoa mingine. Kwa kubaki katika mkoa mmoja ni dalili tosha kabisa Chagga was a weak tribe.

Assume it was a strong tribe, kushindwa kuwashawishi japo mikoa ya karibu kama Tanga, Arusha na Manyara (ambayo ilikuwa part ya Arusha) ili valie zao ziwe shared na makabila jirani, wanajidhihirisha pia walikuwa wabinafsi kwa misingi ya mtoa hoja.

Nyerere kutoka kabila dogo la Wazanaki (ambao wako Butiama na sio Mkoa mzima wa Mara; kama wachaga walivyo shika wiliaya zote z Kili kutoa Mwanga na Pare) kwa Nyerere kuweza kuwaunganisha Makabila yote zaidi ya 130 hata kama Wachaga wangebaki peke yao alijipambanua kama jembe na kiongozi mahiri mwenye kuunganisha watu bila kujali tofauti zao za kikabila unlike Mareale aka Mangi mkuu aliebaki na mkoa mmoa tu.

Aidha nimkubushe tena mtoa hoja, ukubwa wa chiefdom ni uwezo wa kuwa na idadi kubwa ya watu (subjects), kuwa na ardhi kubwa yako na nyingine iliyopatikana kwa chiefdom ku-concur chiefdom zilio-weak. Kwa msingi huo huo, Wachaga kubaki mkoa mmoja wanazidi kudhihirisha walikuwa weak, maana wangekwa strong wange-concur nearby tribes na kukuza influence yao.

Mtoa mada kama ana ufahamu wa kawaida tu, asome ushawishi wa dola ya Babel, Uajemi, Ugiriki, Urumi anaweza kupata walau mwangaza dhana ya tribe supremacy.

So far, 2019 tunategemea Watanzania tujadiliane mijadala ya akili ya what are our common shared values and fight against poverty na sio kupeana hadaa za akina Mangi mkuu as supreme tribe which could be endorsed by the British Governor as a potential leader of Tanganyika. Kama ingetokea (tumshukuru Mungu haikutokea), bila shaka nchi ngejaa ukabila na keki ya Taifa yotee ingekwenda uchagani badala ya Tanganyika yote
 
G
Kwani we Malisa ni mchagga, mimu nilikuwa nafikiri wewe ni mtz
 
Nadhani ni fix tu, maana hakuna kabila la wachaga na wala hakuna lugha ya kichaga.

Waliunganishwa na lugha ipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Juzi nilikuwa kwa wakwe zangu huko juu, aisee nimeenda na hela nimerudi nazo - kuombana hela huko ni so minimal. Sasa ningekwenda kwetu aisee, yaani unaenda benki unachukua mia tano tano na buku buku kabisa kabisa tena zile mpyaaa!! ha ha ha ha

Sidharau kwetu hapana ila najaribu tu kukupa picha ya hali halisi !!
 
Mwalimu alisaidiwa sana na Wazalamo wale wazee wa Mjini wa wakati huo ingawa historia imekaa kimya kidogo kuhusu hili.
 
Inaonekana Malisa kaishiwa siasa
Ni vizuri unavyotupa historia ya Mbokomu Lyamhaa Inn.
 
Ni historia nzuri, nimeipenda. Bila shaka ukoloni ndio uliotuvuruga waafrika vinginevyo tungekuwa mbali.

Hayo maendeleo yote uliyoyasoma pamoja na muundo wa uongozi uliratibiwa na wakoloni........
 
Mkubali ukweli, himaya ya wachaga ilikuwa imepiga hatua, kilichozuia expansionism ya himaya yao ni kwamba tayari mipaka ya Taifa la Tanganyika ilikuwa imeshachorwa tayari. Tuwashukuru wazungu waliotucholea mipaka maana kilichokuwa ninafuata ni makabila yenye nguvu kuyateka makabila dhaifu kama kilichotokea Ethiopia na kilichokuwa kinaendelea Kyle kwa Wazuru. Vita nyingi ya kujitanua kwa kabila ilikoma na mpambano uligeuka dhidi ya wazungu
 
Mwalimu alisaidiwa sana na Wazalamo wale wazee wa Mjini wa wakati huo ingawa historia imekaa kimya kidogo kuhusu hili.
\
Sifa ya komandoo hata wale wa kwenye movie ni uwezo wa kuingia kambi ya adui na kujenga urafiki na wakazi wa hapo ili baadae ajenda yake itimie.
Kwa mwl. Nyerere mtu kutoka Bara, akaweza kuwaunganisha wazaramo akina Sykes na wakamkubali kuwa Chairman wao, hiyo sifa kubwa ya kiongozi kuwashawishi na kuwaunganisha kwa lengo la kumng'oa mkoloni.

Malisa anatupiga sound za a failed tribe even to influence the neighboring region to get rid of British Colonialism
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…