Dola ya wachaga kabla ya uhuru

Dola ya wachaga kabla ya uhuru

Mimi kunaswali mmoja nimekuwa nikijiuliza mara nyingi na mpaka leo sijapata majibu yake, ila naweza pata hapa leo majibu haya!

Hivi wanaojiita wachaga ni kabila moja! na kama ni kabila moja inakuwaje kwa mfano lugha ya mchaga wa machame hailewi mchaga wa Rombo!, kwa ufahamu wangu mimi, watu wa kabila moja lazima wasikilizane, sasa hawa wananichanganya kidogo, au yalikuwa makabila tofauti mtu mmoja au wachache wakafanya jitihada za kuwaunganisha hawa watu na kuwa kabila mmoja ili kutimiza adhma fulani?

Wanaojua jambo hili wanisaidie, niwaombe wachaga msiojua chochote kama mimi kuhusu hili subirini tujifunze wote kwa wachaga wenzenu wanaojua!
Asante.
 
Mwambie huyo mwandishi akajifunze vizuri.
1. Shirika la Ujasusi la Uingereza haliitwi M16 bali ni MI6. Nilidhani ni suala la typo tu lakini kinyume chake naona amerudia makosa yake tena na tena na kuleta maana kuwa kumbe si makosa bali ndiyo uelewa wake.
2. Wachaga si kabila pekee ambalo lilikua limeji establish kwa maana inayosimuliwa, kinachoonekana hapa ni wachaga kuomboleza na kuikumbuka historia ya hali ilivyokuwa miaka ile. Kuna sababu ya kilio chao cha hivi sasa wanapokazana kusimulia historia yao lakini miaka mingine iliyopita hakukuwa na kelele za wachaga kukazana kuandika kama sasa.

3. Kuna story nyingi za kuunga unga ili kuonekana wachaga walikua wanabembelezwa hado kushusha bendera yao ili ya Tanganyika ipande kitu ambacho si kweli.
4. Chief Doms ziliuawa.na hili ni kwa nchi nzima wala hakuna swala la Mangi Mkuu kijiuzuru ili kumpisha Nyerere aongoze. Alijiuzuru sababu hizo Chief Doms ziliachwa bila ya power yoyote ile kimaamuzi. Ndipo wakaleta janja nyingine za kuibukia kwenye vyama vya ushirika navyo wakatumwa watu wa system kwenda kuviua.

Msitake kupotosha watu kwa mambo ambayo hayakuwahi kuwepo.
Tufafanulie hapo pa watu wa system kuuwa vyama vya ushirika tafadhali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama leo kungekuwa na hiyo dola basi ingekuwa ni moja ya nchi maskini sana Duniani..
Mzee unafeli sana.....Kilimanjaro Kingdoms zina special connection Mombasa na Tanga over the centuries..

Kuna handaki/pango underground kutoka Taveta/Rongai mpaka Mombasa kwenye maji na hili ni la centuries.

Hata kama ingekua ni landlocked 100%,nchi ngapi zipo landlocked ni developed?Rwanda,Uganda,etc..

Ni landlocked, Ingekuwa ni nchi ya watu wajinga kuliko wotw, ingekuwa imejaa vita na vurugu za wenyewe wenyewe

Shule na vyuo vipo Moshi tangu 1800's,acha vituko mzee!
 
Mzee unafeli sana.....Kilimanjaro Kingdoms zina special connection Mombasa na Tanga over the centuries..

Kuna handaki/pango underground kutoka Taveta/Rongai mpaka Mombasa kwenye maji na hili ni la centuries.

Hata kama ingekua ni landlocked 100%,nchi ngapi zipo landlocked ni developed?Rwanda,Uganda,etc..



Shule na vyuo vipo Moshi tangu 1800's,acha vituko mzee!
Haya mnayasema kwa sababu ya Neema ya Tanzania...
 
Muandishi na mleta mada naona wote aidha hawana ufahamu wa kutosha wa uongozi na historia ya uongozi ambao ulikuwa na ufanisi na ushawishi ili matakwa yake yakue.

Kama kweli wachaga wangekuwa na nguvu thabiti ya uongozi, basi ilitakiwa wakuze dola yao kutoka mkoa mmoja wa Kilimanjrao na kuleta ushawishi wa utawala wao mikoa mingine. Kwa kubaki katika mkoa mmoja ni dalili tosha kabisa Chagga was a weak tribe.

Assume it was a strong tribe, kushindwa kuwashawishi japo mikoa ya karibu kama Tanga, Arusha na Manyara (ambayo ilikuwa part ya Arusha) ili valie zao ziwe shared na makabila jirani, wanajidhihirisha pia walikuwa wabinafsi kwa misingi ya mtoa hoja.

Nyerere kutoka kabila dogo la Wazanaki (ambao wako Butiama na sio Mkoa mzima wa Mara; kama wachaga walivyo shika wiliaya zote z Kili kutoa Mwanga na Pare) kwa Nyerere kuweza kuwaunganisha Makabila yote zaidi ya 130 hata kama Wachaga wangebaki peke yao alijipambanua kama jembe na kiongozi mahiri mwenye kuunganisha watu bila kujali tofauti zao za kikabila unlike Mareale aka Mangi mkuu aliebaki na mkoa mmoa tu.

Aidha nimkubushe tena mtoa hoja, ukubwa wa chiefdom ni uwezo wa kuwa na idadi kubwa ya watu (subjects), kuwa na ardhi kubwa yako na nyingine iliyopatikana kwa chiefdom ku-concur chiefdom zilio-weak. Kwa msingi huo huo, Wachaga kubaki mkoa mmoja wanazidi kudhihirisha walikuwa weak, maana wangekwa strong wange-concur nearby tribes na kukuza influence yao.

Mtoa mada kama ana ufahamu wa kawaida tu, asome ushawishi wa dola ya Babel, Uajemi, Ugiriki, Urumi anaweza kupata walau mwangaza dhana ya tribe supremacy.

So far, 2019 tunategemea Watanzania tujadiliane mijadala ya akili ya what are our common shared values and fight against poverty na sio kupeana hadaa za akina Mangi mkuu as supreme tribe which could be endorsed by the British Governor as a potential leader of Tanganyika. Kama ingetokea (tumshukuru Mungu haikutokea), bila shaka nchi ngejaa ukabila na keki ya Taifa yotee ingekwenda uchagani badala ya Tanganyika yote
Brilliant
 
DOLA YA WACHAGGA MIAKA MICHACHE KABLA YA UHURU.

By Malisa GJ,

Wakati wazungu wanagawana bara la Afrika, walipokuja walikuta baadhi ya maeneo kuna tawala zenye nguvu, zilizokua na mfumo rasmi wa uongozi. Wao waliziita tawala za jadi (Chiefdoms).

Moja ya tawala iliyokua na nguvu katika ukanda huu wa Afrika Mashariki ni dola ya wachagga (Chagga state). Zilikuwepo nyingine zenye nguvu kama Himaya ya Sultani wa Zanzibar, Dola ya Buganda, Nyamwezi, Ngoni, Haya, Hutu, Tutsi, Hehe, etc.

Dola ya wachagga imetamalaki eneo la pembezoni mwa mlima Kilimanjaro kuanzia maeneo ya Rongai hadi Siha.

Eneo hili lilikua na mtawala mkuu mmoja (aliyeitwa Mangi Mkuu). Huyu alikua kama Rais ama Mfalme wa jamii hiyo. Chini yake walikuwepo watawala wakuu wawakilishi wa majimbo. Hawa waliitwa 'Mangi Waitori'. Chini yao walikuwepo watawala wa wa maeneo madogo, hawa waliitwa Mangi kama vile Mangi Meli wa Old Moshi, Mangi Sina wa Kibosho, Mangi Salakana wa Useri etc.

Kwa mfano eneo kama Rombo lilikuwa na Mangi wengi. Alikuwepo Mangi wa Keni, Mangi wa Mashati, Mangi wa Mengwe etc. Lakini wote waliunganishwa na Mangi Mwitori wa Rombo. Vivyo hivyo katika maeneo ya Kibosho, Machame, Siha, Old Moshi, Marangu etc.

Mangi mdogo aliripoti kwa Mangi Mwitori. Mangi Mwitori naye aliripoti kwa Mangi Mkuu aliyeunganisha wachagga wote.

Kwa mfano kufikia mwaka 1953 Mangi Mwitori wa Vunjo alikua Petro Itosi Marealle, Mangi Mwitori wa Hai alikua Abdiel Shangali, Mangi Mwitori wa Rombo alikua James Selengia Kinabo kabla ya kustaafu mwaka 1952 na John Maruma kuchukua nafasi yake.

Mangi Mwitori alichaguliwa na wamangi wadogo. Kisha wamangi wadogo na wamangi waitori waliunda baraza kuu la uongozi (Supreme council) ambalo lilimchagua Mangi Mkuu.

January 1952 kulifanyika uchaguzi wa kumchagua Mangi Mkuu wa Wachagga. Wagombea walikua watano. Abdieli Shangali wa Machame, Jackson Kitali wa Mbokomu (Old Moshi), Petro Marealle wa Vunjo, John Maruma wa Rombo, na Thomas Marealle wa Marangu.

Baada ya kila mgombea kunadi sera zake, hatimaye kura zilipigwa na Mangi Thomas Marealle kutangazwa mshindi, akifuatiwa kwa mbali na ndugu yake Mangi Petro Itosi Marealle, aliyekuwa Mangi Mwitori wa Vunjo.

Mangi Mkuu ndiye aliyekuwa Kiongozi mkuu wa dola ya wachagga. Baraza la uongozi (Supreme council) ndicho kilikua chombo cha juu kinachosimamia utendaji wa serikali.

Kwahiyo Mangi mkuu alijitahidi sana kushirikiana mangi waitori na mangi wadogo kuhakikisha jamii nzima ya wachagga inajiletea maendeleo.

Kila Mangi alikua na baraza lake la ushauri lililojulikana kama 'baraza la wachili', ambalo lilifanya kazi kama baraza la mawaziri kwa sasa.

Ushirikiano huu ulifanya dola ya Wachagga kupiga hatua kubwa kimaendeleo kuliko jamii nyingi za wakati huo.

Kwa mfano kufikia mwaka 1920 dola ya wachagga ilikua ya kwanza kwenye ukanda wa Afrika Mashariki kuanzisha na kumiliki gazeti lake (Komkya). Miaka 10 baadae dola ya Buganda (Buganda Kingdom) nayo ilianzisha gazeti lake (Buruuli) na mwaka 1940 Himaya ya Sultani wa Zanzibar (Zanzibar Sultanate) nayo ikaanzisha jarida lake (Imperial).

Si hivyo tu, huduma za maji, umeme, miundombinu ya barabara, hospitali na shule vilifika mapema kulinganisha na maeneo mengine ya nchi. Ikulu ya kisasa ya Mangi Mkuu wa wachagga, iliyojengwa karibu miaka 100 iliyopita ndiyo inayotumika hadi sasa kama Ikulu ndogo ya Rais kwa mkoa wa Kilimanjaro.

Zilizokuwa ofisi za watendaji wa serikali ya Mangi mkuu (eneo la KDC Moshi) ndio ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Moshi kwa sasa.

Maendeleo haya na mengine mengi, wachagga waliamini yalitokana na elimu. Kwahiyo mwamko wa elimu ulikua mkubwa hasa baada ya wamisionari kujenga shule na huduma za afya kila walipojenga kanisa. Vitu hivi vitatu viliambatana. Kanisa, Shule, na Kituo cha afya.

Kwahiyo hata kwenye kuchagua viongozi, yule aliyekuwa na elimu nzuri ndiye aliyepewa nafasi kubwa ya kushinda ikiaminika kwamba elimu yake itachochea kasi ya maendeleo. Na hii ni moja ya sababu iliyomfanya Thomas Marealle kushinda kiti cha umangi mkuu mwaka 1952, kwani kati ya wagombea wote yeye ndiye aliyekua na shahada ya uzamili (masters degree) kwa wakati huo.

Kabla ya uhuru kulikua wachumi wawili tu wazawa ambao ni Thomas Marealle na mzee Fredrick Mchauru ambaye walisoma pamoja London School of Economics, kabla ya Marealle kupata ufadhili Cambridge University (Trinity College).

Iliaminika pia kwamba Uingereza ilitaka dola ya wachagga ijitenge kutoka Tanganyika na itafute uhuru wake yenyewe, kama Rwanda na Burundi zilivyojitenga kutoka Tanganyika baada ya vita vya kwanza vya dunia, wakati huo zikiitwa Ruanda-Urundi.

Hata hivyo mpango huo ulishindikana kwa kuwa Tanganyika ilikua 'Trusteeship colony' ya Umoja wa mataifa, na Uingereza alikabidhiwa tu aisimamie hadi iweze kujitawala. Kwahiyo hoja ya Muingereza ilitupwa kwa maelezo kwamba wakati wa kugawanya bara la Afrika pale Berlin mwaka 1984/85 hakuna nchi inayoitwa 'Chagga state' iliyogawanywa. Hivyo uhuru unaopaswa kuwa wa Tanganyika kwa ujumla na sio wa jamii moja moja.

Baada ya jaribio hilo kushindwa, inadaiwa shirika la ujasusi la Uingereza (M16) lilimpendekeza Mangi Thomas Mareale kuwa Rais wa kwanza wa Tanganyika baada ya uhuru.

Katika moja ya barua za Richard Turnbull (Gavana wa mwisho wa Uingereza) kwenda kwa shirika la ujasusi la nchi hiyo (M16) ilieleza mapendekezo hayo kwa Thomas Mareale.

Sehemu ya nyaraka hiyo iliyoandikwa mwaka 1958 ilisema 'I consider Thomas Marreale an outstanding Chagga leader. I dont know him personally but he would be the leader of Tanganyika if British had to leave. However he lack support from other tribes'

Turnbull alikua akiwaelezea M16 kuhusu Mangi Thomas Marealle na umahiri wake katika uongozi. Hata hivyo alionesha hofu kuwa Marealle hakuwa na ushawishi mkubwa kwa makabila mengine nje ya wachagga.

Na hii ni moja ya hofu kubwa aliyokua nayo Mwalimu Nyerere wakati wa kudai uhuru. Alipofika uchaggani alikuta dola ya wachagga ina mamlaka kamili. Ilikua na 'well defined leadership structure', bendera yake, wimbo wake, na askari wake.

Nyerere alisema ili Tanganyika iwe uhuru lazima dola ya wachagga ife kwanza, kwa sababu hatuwezi kuwa na taifa moja ndani ya taifa jingine. Mwaka 1961 Nyerere aliagiza bendera ya Tanganyika isipandishwe kabla bendera ya wachagga haijashushwa kwanza. Tarehe 8 December 1961 saa 5 usiku bendera ya wachagga ilishushwa katika Ikulu ndogo ya Moshi, na muda mfupi baadae (saa 6 usiku, December 9) bendera ya Tanganyika ikapandishwa.

Hata hivyo hofu ya Nyerere haikua na mashiko kwa sababu Mareale mwenyewe alimpa ushirikiano mkubwa wakati wa kudai Uhuru. Na ili kuonesha kwamba hakuwa na mpango wowote wa kumhujumu, aliamua kujiuzulu nafasi yake ya umangi mkuu mwaka 1960, na kuruhusu askari wake kujiunga na jeshi la Tanganyika.

Pichani ni wagombea watatu kati ya watano walioshiriki uchaguzi wa Mangi Mkuu mwaka 1952. Kutoka kushoto ni Mangi Thomas Mareale aliyeshinda uchaguzi huo), Mangi John Maruma (Mangi Mwitori wa Rombo), na Abdieli Shangali (Mangi Mwitori wa Machame).

Malisa GJ
01/01/2019
Moshi.!

Sent using Jamii Forums mobile app
hii umekopy wapi... coz hapo mwishoni unamalizani "PICHANI NI WAGOMBEA WATATU KATI WA WATANO...." lakini hakuna picha.. copy nad paste ndio shider ya wasomi wetu
 
Haya mnayasema kwa sababu ya Neema ya Tanzania...

Mkuu ni kama una chuki na hawa watu.....

Historia aliyotoa ni kabla ya uhuru 1961,sasa sijui unaiunga vipi na current years?

Kila mtu ana heritage yake,yeye katoa ya kwao,sio kwamba akisema kwao pazuri kwako ni pabaya!

Be cool and proud with your heritage...usiwe na chuki bro!

Kama una hoja au una fact toa,sio unakua hater na heritage za watu!

Heritage ni yake,sasa sijui wewe kinakuuma nini?

Na wewe una heritage yako,let everyone of you be happy with your heritages!

These are just histories tu ancestors zake walifanya...sasa sijui unaumia nini?

Watu mna kazi sana!
 
Mkuu ni kama una chuki na hawa watu.....

Historia aliyotoa ni kabla ya uhuru 1961,sasa sijui unaiunga vipi na current years?

Kila mtu ana heritage yake,yeye katoa ya kwao,sio kwamba akisema kwao pazuri kwako ni pabaya!

Be cool and proud with your heritage...usiwe na chuki bro!

Kama una hoja au una fact toa,sio unakua hater na heritage za watu!

Heritage ni yake,sasa sijui wewe kinakuuma nini?

Na wewe una heritage yako,let everyone of you be happy with your heritages!

These are just histories tu ancestors zake walifanya...sasa sijui unaumia nini?

Watu mna kazi sana!
Sina chuki na wachagga, ila ni kweli Wachaga wasingeweza kuwa nchi nje ya Tanganyika
 
Sina chuki na wachagga, ila ni kweli Wachaga wasingeweza kuwa nchi nje ya Tanganyika

Ni sawa,ni wazo lako...tayari ni wishful thinking....

Wenyewe wanaona wangeweza..

Sasa wote mpo entitled with your opinions...

Ila kwa kuwacheck,as per stats,walikua ahead kabla ya 1961...na as of now,jamii yao imeendelea as per stats....This is a FACT!

Sasa,as per my own choice and opinion kati ya hypothesis yao na yako,kura yangu nawapa wao zaidi kuliko wewe kua wangeweza nje ya Tanganyika!

Sijui wewe una stats zipi kunishawishi ku-support your hypothesis?
 
Nyongeza kutoka kwa Kaka Aggrey Marealle kuhusu dola ya Wachagga.
_________________________________

Kila kijiji kilikua na kiongozi (village headman) ambaye alitambulika kama "Mchili". Jumla ya vijiji katika dola ya wachagga vilikua 113. Juu yao kulikua na wamangi (Area Chiefs). Mfano Mangi Sina wa Kibosho, Mangi Salakana wa Useri, Mangi Sabas wa Uru, Mangi Meli wa Old Moshi etc. Jumla yao walikua 17.

Juu yao kulikua na Mangi waitori (Divisional chiefs). Hawa walikua watatu tu kiutawala. John Maruma aliyekuwa Mangi Mwitori wa Rombo, Petro Itosi Marealle Mangi Mwitori wa Vunjo, na Abdieli Shangali Mangi Mwitori wa Hai (Machame).
_
Kila Mwitori alikua na wamangi watano hadi sita chini yake. Na kila Mangi alikua na wachili kadhaa chini yake. Wote hawa walikua chini ya mangi mkuu Thomas Marealle. (Mchili aliripoti kwa Mangi, Mangi aliripoti kwa Mangi Mwitori, na Mangi Mwitori aliripoti kwa Mangi Mkuu).
_
Pichani Mangi Mkuu Thomas Marealle akiwa na binti mfalme, Princess Margaret, October 19 mwaka 1956, wakati Princess Margaret alipomtembelea Ikulu mjini Moshi.!
FB_IMG_1546531571461.jpeg
FB_IMG_1546531495195.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh kwakweli wachaga wapo smart tangu zamani sijui ni kwann watu Wana chuki na watu Hawa
kumbe maendeleo tunayoyaona uchagani yaliasisiwa kitambo
mangi mareale alikuwa moja ya watz 2 kuwa na Masters ya uchumi kabla ya Uhuru,pia walikuwepo wasomi kadhaa include Dr kleruu,nsilo swai etc
jeshini ndio usiseme Vita ya kagera waliokuwa viongoz wa vikosi wengi walikuwa Chagas na pares
example mej jenerali tumainiel kiwelu,Imran kombe, Kimario,brigedia general Benjamin msuya etc
Mungu aendelee kuibariki Kilimanjaro
britanicca
Come27
tinkanyarwele
instanbul
Sky Eclat
Rweye
Frank Wanjiru
chuma cha mjerumani
Otorong'ong'o
Upepo wa Pesa
sikongefdc
last king of uscoch
MBIIRWA
Hawa jamaa wana ujasiri na uthubutu sana
 
Kama leo kungekuwa na hiyo dola basi ingekuwa ni moja ya nchi maskini sana Duniani..
Ni landlocked, Ingekuwa ni nchi ya watu wajinga kuliko wotw, ingekuwa imejaa vita na vurugu za wenyewe wenyewe
Aliyekudanganya nani?umeshawahi kumsikia mchagha akilia lia apate mali za urithi,kama wewe unakaa mjini na siyo kijijini umeshawahi kumuona mchagha ktk hawa wanaookota makopo ya maji wakauze wapate hela za kuvuta cocaine etc?umeshawahi kumuona mwanamke wa kichagha akipitia maduka ya wahindi na waarabu kila ijumaa akiomba omba Tsh 100/200?

Hi ni jamii iliyo active kushinda chochote Mchagha std 7 anamshinda akili Mgogo mwenye degree kichwani.Tena wagekuwa smart kuliko unavyofikiria wewe,by the way ka-google top ten most famous African tribes upate jibu maana nikiandika hapa utasema natetea visivyokuwepo.
 
Aliyekudanganya nani?umeshawahi kumsikia mchagha akilia lia apate mali za urithi,kama wewe unakaa mjini na siyo kijijini umeshawahi kumuona mchagha ktk hawa wanaookota makopo ya maji wakauze wapate hela za kuvuta cocaine etc?umeshawahi kumuona mwanamke wa kichagha akipitia maduka ya wahindi na waarabu kila ijumaa akiomba omba Tsh 100/200?

Hi ni jamii iliyo active kushinda chochote Mchagha std 7 anamshinda akili Mgogo mwenye degree kichwani.Tena wagekuwa smart kuliko unavyofikiria wewe,by the way ka-google top ten most famous African tribes upate jibu maana nikiandika hapa utasema natetea visivyokuwepo.
 
Mimi kunaswali mmoja nimekuwa nikijiuliza mara nyingi na mpaka leo sijapata majibu yake, ila naweza pata hapa leo majibu haya!

Hivi wanaojiita wachaga ni kabila moja! na kama ni kabila moja inakuwaje kwa mfano lugha ya mchaga wa machame hailewi mchaga wa Rombo!, kwa ufahamu wangu mimi, watu wa kabila moja lazima wasikilizane, sasa hawa wananichanganya kidogo, au yalikuwa makabila tofauti mtu mmoja au wachache wakafanya jitihada za kuwaunganisha hawa watu na kuwa kabila mmoja ili kutimiza adhma fulani?

Wanaojua jambo hili wanisaidie, niwaombe wachaga msiojua chochote kama mimi kuhusu hili subirini tujifunze wote kwa wachaga wenzenu wanaojua!
Asante.
Tribe : chagga
Sub tribe: machame, marangu,kibosho , siha etc
Clans: Masawe, mushi, lema,marealle etc
 
Back
Top Bottom