Dola ya wachaga kabla ya uhuru

Dola ya wachaga kabla ya uhuru

Mimi kunaswali mmoja nimekuwa nikijiuliza mara nyingi na mpaka leo sijapata majibu yake, ila naweza pata hapa leo majibu haya!

Hivi wanaojiita wachaga ni kabila moja! na kama ni kabila moja inakuwaje kwa mfano lugha ya mchaga wa machame hailewi mchaga wa Rombo!, kwa ufahamu wangu mimi, watu wa kabila moja lazima wasikilizane, sasa hawa wananichanganya kidogo, au yalikuwa makabila tofauti mtu mmoja au wachache wakafanya jitihada za kuwaunganisha hawa watu na kuwa kabila mmoja ili kutimiza adhma fulani?

Wanaojua jambo hili wanisaidie, niwaombe wachaga msiojua chochote kama mimi kuhusu hili subirini tujifunze wote kwa wachaga wenzenu wanaojua!
Asante.
Hapo hapo nikuulize mkuu.

Watusi na wahutu ni makabila mawili tofauti sio mkuu?

Iweje sasa hao wote wanatumia lugha moja lkn wanakuaje ni makabila mawili tofauti?
 
Hapo hapo nikuulize mkuu.

Watusi na wahutu ni makabila mawili tofauti sio mkuu?

Iweje sasa hao wote wanatumia lugha moja lkn wanakuaje ni makabila mawili tofauti?

Hahahaha, tumalizane na hili la wachaga kwanza, tukimaliza tutahamia na kwa hao wengine nao watuambie ilikuwaje ila sijui kama wako humu jukwaani!
 
Mimi kunaswali mmoja nimekuwa nikijiuliza mara nyingi na mpaka leo sijapata majibu yake, ila naweza pata hapa leo majibu haya!

Hivi wanaojiita wachaga ni kabila moja! na kama ni kabila moja inakuwaje kwa mfano lugha ya mchaga wa machame hailewi mchaga wa Rombo!, kwa ufahamu wangu mimi, watu wa kabila moja lazima wasikilizane, sasa hawa wananichanganya kidogo, au yalikuwa makabila tofauti mtu mmoja au wachache wakafanya jitihada za kuwaunganisha hawa watu na kuwa kabila mmoja ili kutimiza adhma fulani?

Wanaojua jambo hili wanisaidie, niwaombe wachaga msiojua chochote kama mimi kuhusu hili subirini tujifunze wote kwa wachaga wenzenu wanaojua!
Asante.
Hapo kwa kukusaidia tu soma ukurasa wa77 kipengele cha conclusion na recommendation ya research utapata jibu la swali lako, hizo theory zako za kitoto kibaki huko huko vijiweni na siyo huku jukwaani[emoji41][emoji41]

Nimeshindwa upload hiyo document ile link yake hii hapo https://www.researchgate.net/public...eople_in_Kilimanjaro_Region_Tanzania/downloadView attachment TheSourceofLanguageVariationamongChaggapeople.pdf

Sent using Jamii Forums mobile app
 
A
Mwambie huyo mwandishi akajifunze vizuri.
1. Shirika la Ujasusi la Uingereza haliitwi M16 bali ni MI6. Nilidhani ni suala la typo tu lakini kinyume chake naona amerudia makosa yake tena na tena na kuleta maana kuwa kumbe si makosa bali ndiyo uelewa wake.
2. Wachaga si kabila pekee ambalo lilikua limeji establish kwa maana inayosimuliwa, kinachoonekana hapa ni wachaga kuomboleza na kuikumbuka historia ya hali ilivyokuwa miaka ile. Kuna sababu ya kilio chao cha hivi sasa wanapokazana kusimulia historia yao lakini miaka mingine iliyopita hakukuwa na kelele za wachaga kukazana kuandika kama sasa.

3. Kuna story nyingi za kuunga unga ili kuonekana wachaga walikua wanabembelezwa hado kushusha bendera yao ili ya Tanganyika ipande kitu ambacho si kweli.
4. Chief Doms ziliuawa.na hili ni kwa nchi nzima wala hakuna swala la Mangi Mkuu kijiuzuru ili kumpisha Nyerere aongoze. Alijiuzuru sababu hizo Chief Doms ziliachwa bila ya power yoyote ile kimaamuzi. Ndipo wakaleta janja nyingine za kuibukia kwenye vyama vya ushirika navyo wakatumwa watu wa system kwenda kuviua.

Msitake kupotosha watu kwa mambo ambayo hayakuwahi kuwepo.
Akasome vizuri the interim constitution ya 1965
 
Back
Top Bottom