Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
DOME OKOCHI BUDOHI MZALENDO KUTOKA KENYA ALIYEPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA
Naamini umeona hiyo video ya ufunguzi wa kumbi 12 zinazohifadhi historia ya Wakenya katika kupigania uhuru wa nchi yao.
Video hii imenitia hamu ya kumweleza Dome Okochi Budohi.
Sijui kama katika kumbi hizo kuna historia ya Wakenya walioshiriki katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika kama Dome Budohi.
Historia ya Dome Okochi Budohi Mluya kutoka Kenya haiko popote katika historia ya TAA wala ya TANU.
Lakini Dome Budohi ameshiriki katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika kuanzia TAA hadi TANU.
Soma hapo chini uone jinsi nilivyomweleza Dome Budohi katika kitabu cha Abdul Sykes:
''Familia yangu ilifahamiana na Dome Budohi, mmoja wa wanaharakati kutoka Kenya.
Wakati ule wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika alikuwa akiishi Dar es Salaam.
Budohi alikuwa mmoja wa wazalendo walioasisi TANU na kadi yake ya uanachama ni nambari 6 aliyopewa Julai 1954.
Mwaka 1955 alikamatwa na serikali ya kikoloni kwa tuhuma ya kuwa mmoja wa askari wa Mau Mau harakati za wazalendo takriban wengi wao wakulima wadogo waliokuwa wakipigana na ukoloni wa Waingereza nchini Kenya.
Ninazo kumbukumbu nyingi za utoto nikimtembelea Budohi Kituo Cha Kati cha Polisi.
Hivi sasa jengo hilo ni Makao Makuu ya Shirika la Reli la Tanzania. Wakati huo mimi nilikuwa mtoto, si zaidi ya miaka minne hivi.
Jambo la kwanza ninalokumbuka kuhusu Budohi ni kuwa kila mara tulipokwenda kumtembelea tulimkuta anasoma gazeti.
Baadae Budohi alihamishiwa Kenya na aliwekwa kizuizini katika kisiwa cha Lamu.
Alipofunguliwa toka kizuizini mwaka wa 1963 miezi michache kabla ya uhuru wa Kenya, Budohi alikwenda Uganda na akaajiriwa na gazeti la Uganda Argus.
Hivi sasa ninaelewa kwa nini siku zile kila mara nilikuwa namkuta amezama ndani ya gazeti kila tulipokwenda kumtembelea pale rumande mjini Dar es Salaam.
Niliweza kwa msaada wa rafiki yake Maxwell aliyelowea Tanganyika, kumpata Budohi mjini Nairobi mwaka 1972.
Nilimtembelea mjini Nairobi wakati huo alikuwa akiishi Ruiru maili chache kutoka Nairobi mjini.
Budohi alikuwa ametundika picha ya Nat King Cole sebuleni kwake.
Mwaka 1974 nilimtembelea tena, safari hii katika nyumba yake ya Ngei Estate.
Budohi alikuja kuwa mtu wa kwanza kabisa kunipa habari kuhusu historia ya harakati za Tanganyika dhidi ya ukoloni wa Waingereza.
Hata hivyo wakati ule nilikuwa bado sijapata hamu wala kuwa na hamu ya kuandika kitabu kuhusu uhuru wa Tanganyika.''
Picha ya pili ni Mzee Maxwell na mwandishi picha hii tulipiga katika miaka ya 1990 Mtaa wa Mafia karibu na Msikiti wa Manyema na picha ya tatu ni Dome Budohi na mwandishi, Ruiru Nairobi, 1972.