SoC01 Domestic workers ni ajira inayohitajika sana Oman, kuna umuhimu wa kuiboresha

SoC01 Domestic workers ni ajira inayohitajika sana Oman, kuna umuhimu wa kuiboresha

Stories of Change - 2021 Competition

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Wasaidizi wa ndani wanahitajika duniani kote. Nchi za Magharibi zimeboresha mikataba na maslahi ya wafanya kazi wa ndani, matokeo yake ni wachache wenye uwezo wa kuajiri wafanya kazi hao. Hao wachache wanaopata ajira wana mikataba ya kazi, likizo kila mwaka, malipo wakiwa wagonjwa, kiinua mgongo na mishahara inayo wawezesha kumudu gharama za maisha.

Oman na nchi za Kiarabu wanatoa ajira sana za wafanyakazi wa ndani kutoka Tanzania. Bahati mbaya kuna wanaopitia mateso. Wengine mpaka mauti yanawakuta. Hii imefanya mpaka Serikali kufanya upatikanaji wa ajira hizi kuwa mgumu.

Si wote wanapata mateso na kurudi nyumbani bila mafanikio. Kuna binti ninaemfahamu aliweza kuwajengea wazazi wake nyumba, kusomesha watoto na kupata mtaji wa kibiashara chake kutokana na ajira yake Oman iliyodumu kwa miaka 10.

Tatizo la ajira nchini ni kubwa sana. Kuna haja ya Serikali kufikiria jinsi ya kushirikiana na Serikali za nchi kama Oman. Kupitia Balozi zetu, wabobezi wa Human Resources na wanasheria waandae mikataba yenye tija kwa raia wetu.

1. Mwajiri alazimike kukata bima itakayofidia nauli ya mwajiriwa kama kutatokea manyanyaso.

2. Kuwe na HR officer Ubalozini atakayesikiliza kero za wafanyakazi, awe na uwezo wa kuongea na waajiri kama mwakilishi wa wafanyakazi.

3. Ajira zote zipitie Ubalozini na ikiwezekana Balozi ziweke matangazo kwenye redio na runinga kuwa wanaweza kukupatia wafanyakazi.

Kama kila ajira, $10 kila mwezi itabaki ubalozini, itafidia gharama za uendeshaji wa zoezi zima.
 
Upvote 13
Very rare cases.... na zaidi UBALOZI upo, na Agent (wakala halali wanae unganisha mwajiri na muajiriwa wapo nchi zote mbili) mkataba upo..
Sasa tatizo lipojee?
 
Kama huna professional achana ns hizo kazi za ndani huko middle east yote ngozi yetu haipendwi sana huko wazungu hawatupendi ila angalau wao
 
Kama huna professional achana ns hizo kazi za ndani huko middle east yote ngozi yetu haipendwi sana huko wazungu hawatupendi ila angalau wao
Cuba wana export madaktari na Philippines wana export manesi. Sisi hakuwekeza kwenye elimu kwahiyo uwezo wetu ni ku export domestic workers.
 
Mimi nisinge encourage watu kwenda huko mkuu,story za huko ni za kutisha,ila kwa kuwa watu wabishi sana pesa inawalazimu ku risk maisha yao then naafiki kuwe na improvement kwenye hizo ajira ku minimize risks...
 
Wengi naowafahamu waloenda huko wamefanikiwa kiasi!
 
Cuba wana export madaktari na Philippines wana export manesi. Sisi hakuwekeza kwenye elimu kwahiyo uwezo wetu ni ku export domestic workers.
Hii sio njia sahihi kama tumeshindwa zalisha pro tukomae nao hapa hapa middle east sio juzi kuna kiroba toka Dubai kimetua jnia maswala ya kazi za ndani na serikali zao zina walinda walio fanya huo uhalifu
 
Mimi nisinge encourage watu kwenda huko mkuu,story za huko ni za kutisha,ila kwa kuwa watu wabishi sana pesa inawalazimu ku risk maisha yao then naafiki kuwe na improvement kwenye hizo ajira ku minimize risks...
Kukosekana kwa ajira katika nchi za Afrika baada ya uhuru hakuna miradi mingi iliyoanzishwa na kutoa ajira kwa wingi, hili ni tatizo kubwa linalofanya vijana kukimbilia Ulaya na Arabuni kufanya kazi za kitumwa. Watu wanaondoka kwa desperation. Ni kheri kama kuna njia ya kuboresha ili iwe ya uwazi na maovu yaepukwe.
 
Wote mnaonesha upande mmoja wa shilingi!!
Kwanini hamuoneshi upande wa pili?
Pia wapo wengi wamefaidika na kunufaika kiasi wamejenga nyumba huku TZ na wamenunua mashamba , viwanja kwa muda mfupi tu waliyotumika huko ughaibuni....
Laa ajabu madhila yanawakuta wadada wajanja wanaotaka short cut ( njia ya mkato kwa kujihusisha X na watume za wenye nyumba )
 
Tokea yule dada alikuwa mchepuko wangu kunambia kurudi Oman sasa anatowa mpaka kisamvu. Kuna la kujifunza sana

Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Kukosekana kwa ajira katika nchi za Afrika baada ni tatizo kubwa linalofanya vijana kukimbilia Ulaya na Arabuni kufanya kazi za kitumwa. Watu wanaondoka kwa desperation. Ni kheri kama kuna njia ya kuboresha ili iwe ya uwazi na maovu yaepukwe.
Hili la ajira ni uzembe tu wa watu waliopo serikalini tu afrika tunaweza tengeneza ajira nyingi sana mfano India ilitengeneza ajira zaid ya elfu kumi kwa tanzanite inayochimbwa pale arusha tu
 
sawa,lakini na story za maltreatment ziko huko Arabuni sana kuliko sehemu nyingine
Da Rebeca... just let us be Fair ...
Mbona wavulana na me hayawakuti hayo!!
Sista wengi hujilegeza huko kwa waBaba na vijana wao barubaru.. sasa inapogundulika heshima inapotea.. na unyanyasaji na madhila huibuka !!!!!
 
Kukosekana kwa ajira katika nchi za Afrika baada ni tatizo kubwa linalofanya vijana kukimbilia Ulaya na Arabuni kufanya kazi za kitumwa. Watu wanaondoka kwa desperation. Ni kheri kama kuna njia ya kuboresha ili iwe ya uwazi na maovu yaepukwe.

i agree,ila Uarabuni hawatupendi weusi ila lazima watu wapewe informations zote what to expect huko, i bet out of desperation hata uwaambie nini bado wataenda,..it is sad,
 
sawa,lakini na story za maltreatment ziko huko Arabuni sana kuliko sehemu nyingine
Walio fanikiwa ni wachache sana tena wanarudi wakiwa na maisha ya kawaida tu kama wengine tu huku uswahilini ila wanaopata majanga ni wengi
 
Hili la ajira ni uzembe tu wa watu waliopo serikalini tu afrika tunaweza tengeneza ajira nyingi sana mfano India ilitengeneza ajira zaid ya elfu kumi kwa tanzanite inayochimbwa pale arusha tu
Baada ya WWII Holland walijenga kiwanda cha vitenge ili kuzalisha ajira kwa vijana wao. Soko la vitenge hivyo ni Afrika.
 
Da Rebeca... just let us be Fair ...
Mbona wavulana na me hayakuti hayo!!
Sista wengi hujilegeza huko kwa waBaba na vijana wao barubaru.. sasa inapogundulika heshima unapotezea.. na unyanyasaji na madhila huibuka !!!!!
Wapo wanaopata madhira pia wengi wanaona aibu kusema kama wamepakuliwa kisamvu ila number ya Wavulana inapungua siku hadi siku
 
Sky nawewe unataka million tano za jf ,Mbowe hawalipi siku hizi mishahara yenu? Bure kabisa
 
Da Rebeca... just let us be Fair ...
Mbona wavulana na me hayakuti hayo!!
Sista wengi hujilegeza huko kwa waBaba na vijana wao barubaru.. sasa inapogundulika heshima unapotezea.. na unyanyasaji na madhila huibuka !!!!!

wengi wanaofanya kazi za ndani ni wanawake mkuu,so uwiano hauko sawa, i agree wanaweza kujilegeza lakini pia na wababa wa huko kutaka kutake advantage.....pia mtu akikosea si unampa adhabu ndogo tu..story za huko adhabu zake ni za kutisha eti
 
Back
Top Bottom