SoC01 Domestic workers ni ajira inayohitajika sana Oman, kuna umuhimu wa kuiboresha

SoC01 Domestic workers ni ajira inayohitajika sana Oman, kuna umuhimu wa kuiboresha

Stories of Change - 2021 Competition

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Wasaidizi wa ndani wanahitajika duniani kote. Nchi za Magharibi zimeboresha mikataba na maslahi ya wafanya kazi wa ndani, matokeo yake ni wachache wenye uwezo wa kuajiri wafanya kazi hao. Hao wachache wanaopata ajira wana mikataba ya kazi, likizo kila mwaka, malipo wakiwa wagonjwa, kiinua mgongo na mishahara inayo wawezesha kumudu gharama za maisha.

Oman na nchi za Kiarabu wanatoa ajira sana za wafanyakazi wa ndani kutoka Tanzania. Bahati mbaya kuna wanaopitia mateso. Wengine mpaka mauti yanawakuta. Hii imefanya mpaka Serikali kufanya upatikanaji wa ajira hizi kuwa mgumu.

Si wote wanapata mateso na kurudi nyumbani bila mafanikio. Kuna binti ninaemfahamu aliweza kuwajengea wazazi wake nyumba, kusomesha watoto na kupata mtaji wa kibiashara chake kutokana na ajira yake Oman iliyodumu kwa miaka 10.

Tatizo la ajira nchini ni kubwa sana. Kuna haja ya Serikali kufikiria jinsi ya kushirikiana na Serikali za nchi kama Oman. Kupitia Balozi zetu, wabobezi wa Human Resources na wanasheria waandae mikataba yenye tija kwa raia wetu.

1. Mwajiri alazimike kukata bima itakayofidia nauli ya mwajiriwa kama kutatokea manyanyaso.

2. Kuwe na HR officer Ubalozini atakayesikiliza kero za wafanyakazi, awe na uwezo wa kuongea na waajiri kama mwakilishi wa wafanyakazi.

3. Ajira zote zipitie Ubalozini na ikiwezekana Balozi ziweke matangazo kwenye redio na runinga kuwa wanaweza kukupatia wafanyakazi.

Kama kila ajira, $10 kila mwezi itabaki ubalozini, itafidia gharama za uendeshaji wa zoezi zima.
 
Upvote 13
i agree,ila Uarabuni hawatupendi weusi ila lazima watu wapewe informations zote what to expect huko, i bet out of desperation hata uwaambie nini bado wataenda,..it is sad,
Kama ni rangi nyeusi ??? FYI, uarabuni kuna 50/50% Weusi wapo na kila rangi ipo na kila Taifa la ulimwenguni wapo wamezaliana kibao!!
Wapo hata waFalme weusi...
 
Kama ni rangi nyeusi ??? FYI, uarabuni Luna 50/50% Weusi wapo na kila rangi ipo ns kila Taifa la ulimwenguni wapo wamezaliana kibao!!
Wapo hata waFalme weusi...

Okay maybe uko huko una experience nao,sasa kwa nini hizo race nyingine hatusikii zikiadhibiwa kama ngozi nyeusi...???... huoni kama huu ni ushahidi hawatupendi??
 
Okay maybe uko huko una experience nao,sasa kwa nini hizo race nyingine hatusikii zikiadhibiwa kama ngozi nyeusi...???... huoni kama huu ni ushahidi hawatupendi??
My dear Rebeca..... huku kila kabila geni linalaumu wenyeji... na wenyeji wanalaumu wageni.. ( human nature) ukirudi nyuma utaona hata wa mjini kulaumu wakijijini
Na wakijiji hulaumu wa mjini..

Infact kweli zipo cases na cases.. true sikatai ila Ubalozi upo na vyombo vya utetezi wa haki zipo... (international human watch nk nk )
Sasa turudi home jee beki3, wadada wanaotumikishwa king'ono wanamlilia dannii poor vibinti vinaletwa mjini bila kutambua....
God forbid..
 
Mzee mwenzangu naona unalichukulia lightly hili swala, so kama tanzania wapo housegirls wananyanyaswa then ni sawa wadada kunyanyaswa uarabuni???...

.labda kuna ubalozi na vyombo vya utetezi ila vimekuwa wapi mpaka tunashuhudia watu wakijeruhiwa vibaya???....mwenzangu kuna tatizo mahali..hatuwezi kulifunika funika,lazima kuwe na transparent hiring proccesses...waajiri wajulikane na wawe responsible kukitokea tatizo
 
Fundamentally agreed... as binaadamu naona uchungu na inauma Kuona mtu, binadamu kuonewa au kudhuriwa..... Honestly sipendi.

Tujifunze kwa wale waliyorudi na mafanikio yaani upande wapili wa coin..
Wizara,nchi zikaae kulizungumza na kuleta tija!!!!
Masilahi pande zote zitapatikana.
 
My dear Rebeca..... huku kila kabila geni linalaumu wenyeji... na wenyeji wanalaumu wageni.. ( human nature) ukirudi nyuma utaona hata wa mjini kulaumu wakijijini
Na wakijiji hulaumu wa mjini..

Infact kweli zipo cases na cases.. true sikatai ila Ubalozi upo na vyombo vya utetezi wa haki zipo... (international human watch nk nk )
Sasa turudi home jee beki3, wadada wanaotumikishwa king'ono wanamlilia dannii poor vibinti vinaletwa mjini bila kutambua....
God forbid..
Kuhusu hili la dada wakazi nyumbani kwakweli inasikitisha sana. Ingawa utumwa ulikwisha takriban miaka 200 iliyopita lakini Afrika utumwa bado una endelea tena kwa wa Afrika wenzetu.
 
Matukio mengi ya kutisha yanatokea Saudi Arabia, huko inaelekea wana roho mbaya sana dhidi ya Waafrika. Doha (Qatar) na Dubai wako Wakenya wengi pia na Waganda ambao wamefanyiwa mipango ya kwenda huko na Employment Agents toka nchi zao. Niliwakuta wengi Airports. Oman sijasikia matukio ya kutisha labda yapo lakini hayaripotiwi.
Mimi nisinge encourage watu kwenda huko mkuu,story za huko ni za kutisha,ila kwa kuwa watu wabishi sana pesa inawalazimu ku risk maisha yao then naafiki kuwe na improvement kwenye hizo ajira ku minimize risks...
 
Demand na Supply...

Sasa hivi huenda Demand ni kubwa sana kwa kina dada toka Tanzania sababu ya urahisi, kutokuwa na mikataba na gharama anayolipa muhitaji....

Je Baada ya kuongeza cost ya mikataba, hio USD 10 ya kubaki ubalozini n.k. bado demand itakuwa kubwa au hao waajiri na watesaji watahamia kwenye kina dada wengine wasio na mikataba n.k?

Hii ni ngumu kufanywa na government / ubalozi directly ila wewe kama unaona fursa unaweza ukaanzisha kampuni ya kuwapeleka wafanyakazi huko na kuwapa hizo guarantee zote na kuhakikisha hawawi abused..., ili ikitokea shida ndugu za hao wafanyakazi waweze kukuwajibisha, au wakipata shida huko waweze kukimbilia kwako, pia utakuwa unafanya due dilligence kuhakikisha huwapeleki wakawe sex slaves.
 
Wote mnaonesha upande mmoja wa shilingi!!
Kwanini hamuoneshi upande wa pili?
Pia wapo wengi wamefaidika na kunufaika kiasi wamejenga nyumba huku TZ na wamenunua mashamba , viwanja kwa muda mfupi tu waliyotumika huko ughaibuni....
Laa ajabu madhila yanawakuta wadada wajanja wanaotaka short cut ( njia ya mkato kwa kujihusisha X na watume za wenye nyumba )
Umeongea ukweli. Watu wamekariri uarabuni ni mateso tu.
 
Wanalipwa vizuri tofauti na huku
Ulaya na Arabuni, ajira za kazi za ndani unalipwa kima cha chini cha mshahara. Gharama za makazi ziko juu, ukijitegemea hela nyingi inaishia kwenye pango. Waajiri wengine wanatoa makazi lakini chakula unajitegemea, hii si mbaya kwani bei ya chakula si kubwa sana. Wengine wanakupa Malazi na chakula.
 
Ulaya na Arabuni, ajira za kazi za ndani unalipwa kima cha chini cha mshahara. Gharama za makazi ziko juu, ukijitegemea hela nyingi inaishia kwenye pango. Waajiri wengine wanatoa makazi lakini chakula unajitegemea, hii si mbaya kwani bei ya chakula si kubwa sana. Wengine wanakupa Malawi na chakula.
Fact.... zaidi kuwa tips (bakhshishi) huongeza kipato cha mfanyakazi yaani ukiwa smart na msikivu unapewa Dinar/pesa/riyals,$$ na wanafamilia ktk kila tukio, munasaba Siku za sikukuu, Harusi, birthdays nk nk ukichapa kazi extra yard..unafurahishwa kwa tips ..
 
Safi kama una connection huko toa kwa vijana na wazee tuende tukapige kazi.
 
Back
Top Bottom