Dona iliwe na nini ipendeze mdomoni

Dona iliwe na nini ipendeze mdomoni

vamda

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
895
Reaction score
571
Ndugu wadau. Napenda kufahamu mboga/ kitoweo gani kinapendeza kulia ugali wa dona.
 
Ndugu wadau. Napenda kufahamu mboga/ kitoweo gani kinapendeza kulia ugali wa dona.

Upate samaki wa jodari au sangara aungwe na tui la karanga..nakumbuka pale Morogoro kuna sehem panauzwa chakula asili..
 
kula na dagaa, samaki au nyama iliyokaangwa au rlosti na mboga za majani. usile na maharage, kunde na jamii ya kunde
 
samaki, kama ni mpenzi wa maharage inapanda vile vile, mlenda kama ni mtumiaj. kwa upande wangu hakuna mboga mbaya ni mapishi tu yanagomba mkuu
 
Kula na mlenda wa karanga na Samaki alokaangwa au rosti ya nyama...
 
Huwa nakumbukaga sana ugali maharage wa mama home. Huwa sisahau
 
  • Thanks
Reactions: Mom
Kula na dagaa uono walopikwa kwa nazi kwa tui bubu.
 
nenda kajifunze tabora kwa wanyamwezi, kuna mremnda waommoja wa majani makavu wakitia karanga, kombe la mtindi pembeni na nyamachoma cya kutafunia....saafi! btw, mi napenda wa mtama na samaki.
 
wale dagaa wa ziwa nyasa ni noma kuchemka nilichoka kbs
 
Ngoja tusaidiane ktk hili., hata mimi dona nilikia siwez kulila kwa sababu lilikua linajaa mdomon yan halimezeki hata ule na mboga gani. Sasa bas nilivyosaga tena ule unga wang wa dona nkachanganya na unga wa muhogo bas ikasaidia kuufanya uwe mlaini. Lakin pia kuna baadhi ya mashine zetu za kisaga zinapenyesha nafaka kitu ambacho kinasababisha ule unga uwe na punje nene na ukila haupendez mdomom. Sasa bas sio tatizo ukishasaga unga wako uchekeche ili utoe yale mapunje yasiyosagika vzr na ni vzr uchanganye na unga wa muhogo kwan unafanya dona lako liwe lain mkonon mpk mdomon kwako. Hapo sasa waweza kulila kwa mboga yeyote utayoipenda kwa wkt huo.
 
Mimi napenda na mboga za majani. Mchicha, majani ya maboga, spinachi, kisamvu cha karanga/kweme, mnavu you name it. Labda na samaki mkavu pembeni, mboga ya mchuzi siwezi kulia kabisa.
 
Maziwa mgando ambayo hayajakuwa machachu sana. Halafu ukute mahindi yalikuwa matamu, utakula usinzie. Not healthy sio ule kila siku.
 
Mbona dona ni nzuri tu na ina taste nzuri mdomoni kuliko hata sembe(sio ya ranger,chonji au teves,hii ya bakhresa),mie napenda kula dona na samaki wa sangara minofu(kukaanga sio wa mchuzi) sh 14,000 kwa kilo supermarket na maarage ya njano yalioungwa na nazi.
 
Back
Top Bottom