Joseverest
JF-Expert Member
- Sep 25, 2013
- 52,812
- 71,392
sawa tusubiri mtaniTutamtumia kichuya kuwaua mapema iwezekanavyo!!!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
sawa tusubiri mtaniTutamtumia kichuya kuwaua mapema iwezekanavyo!!!!
imeshindikana mtani...tafuteni mwinginekweli pole yetu. nilikua namtamani sana atue Msimbazi.
Hata Niyonzima bado hajasajili Simba..Akihojiwa na Sports HQ ya EFM leo Kaburu wa Simba amesema maneno kuwa Niyonzima amesajiliwa Simba hata yeye anayasikia mtaani.Tuliambiwa mmewasajili Ngoma na Niyonzima
Umeambiwa na Kaburu au Mwenyekiti wa kamati ya usajili?Tuliambiwa mmewasajili Ngoma na Niyonzima
Kaburu yupo ndani anahojiwa na TakukuruUmeambiwa na Kaburu au Mwenyekiti wa kamati ya usajili?
Acha kuamini kila neno
Wewe si ndio ulituambia mmemsajili Niyonzima ?Umeambiwa na Kaburu au Mwenyekiti wa kamati ya usajili?
Acha kuamini kila neno
Ndiyo lakini si Ngoma..!Wewe si ndio ulituambia mmemsajili Niyonzima ?
Bado kwa Haruna LipumbaYanga yamsajili Donald Ngoma
Simba yamsajili Msondo Ngoma
Laughs moreHe who laughs last.....
Mkuu, hapo umeua!Yanga yamsajili Donald Ngoma
Simba yamsajili Msondo Ngoma
Okwi ana mafanikio gani kumzidi Ngoma?NGOMA ni mchezaji wenu wana Yanga African. mnashangilia kama mchezaji bora kama level za Okwi . Sisi Ngoma anahusiana na nn kwenye chama letu? Msimu mzima kacheza mzunguko wa kwanza tu.
Nimecheka sanaYanga yamsajili Donald Ngoma
Simba yamsajili Msondo Ngoma
Bado Niyonzima tuheshimiane hapa mjiniView attachment 531882
Kuna tetesi kwamba Donald Ngoma atania saini kwenye form za usajiri za Yanga mchana huu ili kuendelea kuitumikia Yanga,pia taarifa zinaendelea kusema kwamba,kiungo wa kati wa Yanga aliyevumishiwa kusaini Simba Haruna Niyonzima nayeye pia kaamua kujirudisha Yanga ili wakae mezani upya na kama watashindwana basi haoni sababu ya kuichezea timu nyingine ya Tanzania,na badala yake atafungasha virago vyake na kurejea kwao.
Taarifa zaidi zitafuatia.
======
UPDATES:
======
ATTACH=full]532001[/ATTACH]View attachment 532026 View attachment 531882 View attachment 531878 View attachment 532001
Na Mahmiud Zubeiry, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Zimbabwe, Donald Dombo Ngoma amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga SC.
Ngoma aliwasili jana usiku Dar es Salaam baada ya taarifa kwamba amesaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na Polokwane City ya Afrika Kusini.
Lakini tangu jana mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amekuwa kwenye mazungumzo na uongozi wa Yanga kabla ya leo mchana kusaini, hivyo pia kuzima tetesi za kwamba anataka kujiunga na mahasimu, Simba.
Katika miaka yake miwili ya kwanza, Ngoma alikuwa ana msimu wa kwanza mzuri Yanga SC, akiiongoza kutwaa mataji yote matatu, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), au Azam Sports Federation Cup (ASFC) na kuiwezesha pia kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, baada ua kutolewa 16 Bora Ligi ya Mabingwa.
Hata hivyo, msimu wake wa pili Ngoma hakuwa mzuri Yanga kutokana na kusakamwa na maumivu ya goti, huku timu yake ikiweza tu kutetea taji Ligi Kuu na kuvuliwa mengine ya Ngao ya Jamii iliyochukuliwa na Azam na ASFC lililobebwa na Simba.
Na hata katika michuano ya Afrika, Yanga haikuweza kurudia mafanikio yake ya msimu uliopita baada ya kushindwa kufuzu hatua ya makundi.
Ngoma aliyezaliwa Kwekwe, Zimbabwe alijiunga na Yanga SC mwaka 2015 akitokea FC Platinum ya kwao, aliyoanza kuichezea mwaka 2012 akitokea Monomotapa United iliyomuibua mwaka 2011.
Amewahi kuitwa timu ya taifa ya Zimbabwe mara kadhaa tangu mwaka 2011na hadi sasa amecheza mechi nane na kufunga mabao matatu. Na kwa kusaini Yanga, maana yake ataendelea kufanya kazi na rafiki zake, kiungo Mzimbabwe Thabani Kamusoko na mshambuliaji Mzambia, Thabani Kamusoko
Makofia Hans Pope alikuwa anajinasibu kuwa wameshamalizana na Haruna na wako mbioni kumalizana na NgomaUmeambiwa na Kaburu au Mwenyekiti wa kamati ya usajili?
Acha kuamini kila neno
Mmmhh,, na zile taarifa za Ngoma kusaini miaka mitatu Polokwane fc ya south vipi??