Donald Ngoma kukaa nje ya uwanja muda usiojulikana

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
ngoma 34.jpg
Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Yanga Donald Ngoma ataendelea kuwa nje ya uwanja kwa muda usiojulikana baada ya kuumia kwenye mechi ya ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar na jana asubuhi Oktoba 2 akashindwa kuendelea na mazoezi.

Msemaji wa Yanga Dismas Ten amesema kuwa bado wanasubiri ripoti ya daktari wa timu Dr. Edward Bavu ili kujua ni muda gani Ngoma atakaa nje.

Dismas ameongeza kuwa daktari Bavu amethibitisha kuwa ripoti hiyo inaweza kutoka ndani ya saa 48 zijazo baada ya kumfanyia uchunguzi wa kina nyota huyo raia wa Zimbabwe.

Donald Ngoma alishindwa kufanya Mazoezi asubuhi ya jana kufuatia maumivu misuli ya paja aliyoyapata kwenye mchezo uliopigwa Jumamosi dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo timu hizo zilitoka sare. Mchezo wa Yanga unaofuata utakuwa dhidi ya Kagera Sugar tarehe 14/10/2017 Kwenye uwanja wa Kaitaba.

Chanzo: EATV
 
Hapa Yanga akipona tumuuze manake majeraha hayataisha kwa sasa na akigusa miaka 30 ndo kabisa huku mshahara akiwa anachukua mkubwa, ametoa mchango wake mkubwa na tunautambua...kwanini hukuuzwa alipohitajika Egypt kama tulivofanya kwa Msuva..? Anyaway ugua pole Mungu atakuponya.
 
Msuva katoka Yanga akiwa huru.
 
Msuva aliuzwa na Yanga, hakuwa huru ndugu, uliza vizuri kwanini yanga walipata sh 177m!!
 
Hapa Yanga akipona tumuuze manake majeraha hayataisha kwa sasa na akigusa miaka 30 ndo kabisa huku mshahara akiwa anachukua mkubwa, ametoa mchango wake mkubwa na tunautambua...kwanini hukuuzwa alipohitajika Egypt kama tulivofanya kwa Msuva..? Anyaway ugua pole Mungu atakuponya.
Wewe ni kiongozi? Au ni kidampa tu? Ulitoa shilingi ngapi kuchangia usajili wake hadi uanze kufikiria kuuza? Pesa ya mshahara unatoa?
 
Wanavotuambia kuchangia timu na kadi ya uanachama kama huchangiaji ni shauri yako ..ushauri tu mbona unapanic...kiwango cha huyo mchezaji wetu unakiona kiko vizuri au huangalii mpira?
 
Title na habari yenyewe havina uhusiano.
Muda wa kuwa nje ni mpaka taarifa ya Daktari lakini title inaonyesha atakuwa nje muda mrefu
 
Hapo andika maumivu tuu ila Ajibu Migomba (pandikizi) atawasaidia
 
Back
Top Bottom