Kwa wale ambao wamekuwa wakifuatilia habari za kimataifa usiku wa kuamkia leo, mtakubaliana nami kwamba dunia ilikuwa ukingoni mwa Vita vya Tatu vya Dunia (WW3). Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali kama Al Jazeera, The Guardian na mashirika mengine makubwa, hali ilikuwa tete sana kati ya Marekani (chini ya Rais Donald Trump) na Iran.
Hapa nimewaletea muhtasari wa kile kinachoendelea, masuala makuu ya kuzingatia, na tafsiri yake katika ulingo wa siasa za kimataifa na athari zake kwetu.
NINI KIMETOKEA?
Rais Trump alikuwa ametoa Ultimatum (makataa) makali sana kwa Iran kwamba wafungue Mlango wa Bahari wa Hormuz (Strait of Hormuz), la sivyo Marekani ingeshambulia na kusambaratisha miundombinu yote ya kiraia na kijeshi ya Iran. Trump alitumia maneno mazito akisema: "A whole civilization will die tonight."
Hata hivyo, zikiwa zimesalia chini ya saa mbili kabla ya makataa kumalizika, Trump alibadili msimamo na kutangaza kupitia mtandao wake wa Truth Social kwamba amekubali Ceasefire (Usitishaji mapigano) wa wiki mbili.
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA
1. Usuluhishi wa Pakistan: Usitishaji huu wa mapigano umewezekana kufuatia diplomasia ya dakika za lala salama iliyoongozwa na Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif. Pakistan sasa itakuwa mwenyeji wa mazungumzo kati ya Marekani na Iran huko Islamabad kuanzia Ijumaa.
2. Kufunguliwa kwa Strait of Hormuz: Sharti kuu la Marekani lilikuwa mlango huu, ambao unapitisha 20% ya mafuta yote duniani, ufunguliwe. Iran imekubali kuufungua kwa wiki mbili, lakini chini ya usimamizi wa jeshi lake, jambo linaloibua maswali ya kiusalama.
3. Mpango wa Pointi 10 wa Iran: Iran haijasalimu amri mikono mitupu. Imewasilisha masharti 10 yanayotaka Marekani kuondoa majeshi yake kikanda, kuondoa vikwazo vya kiuchumi (sanctions), kutoa fidia, na kuruhusu mpango wao wa nyuklia/Urani. Cha kushangaza, Trump ameita mpango huu "workable" (wa kufanyia kazi) huku akijitangazia "Ushindi wa 100%".
4. Wasiwasi wa Uhalifu wa Kivita (War Crimes): Tishio la Trump kushambulia madaraja, vituo vya umeme na raia liliibua hofu kubwa Umoja wa Mataifa (UN) na kwa wanasheria wa kimataifa, wakitahadharisha kuwa huo ungekuwa uhalifu wa kivita.
TATHMINI: TAFSIRI YAKE NI NINI?
Mkwara wa Trump au Nguvu ya Iran? Pande mbili za wachambuzi zinavutana. Wapo wanaosema Trump ametumia mbinu ya "Madman Theory" (kutoa tishio la kicha na la kuogofya) ili kuwalazimisha Iran kufungua bahari na kurudi mezani. Kwa upande mwingine (wafuasi wa Pro-Iran), wanasema Trump amehofia uwezo wa kijeshi wa Iran na maafa ya kiuchumi yatakayotokea nchini mwake na Ulaya, hivyo akaufyata dakika za mwisho.
Athari kwa Nchi Zinazoendelea (Kama Tanzania): Suala la Strait of Hormuz ni la kiuchumi zaidi. Kabla ya makubaliano haya, bei ya mafuta kwenye soko la dunia ilikuwa inapaa kwa kasi. Kwa nchi yetu, vita ingesababisha mfumuko mkubwa wa bei za bidhaa mtaani. Kuwepo kwa Ceasefire kumeshusha presha kwenye masoko ya nishati; hivyo, mwananchi wa kawaida anaepuka makali haya kwa sasa.
Kushuka kwa Ushawishi wa Ulaya: Katika mgogoro huu, mataifa ya Ulaya yameonekana kukosa sauti, wakati nchi za Asia (China katika kushawishi chini kwa chini, na Pakistan katika usuluhishi wa moja kwa moja) zikichukua usukani. Huu ni mabadiliko makubwa ya kidiplomasia duniani (Shift in Global Geopolitics).
Muda wa Wiki Mbili (Ticking Time Bomb): Wiki mbili ni muda mfupi sana kutatua mgogoro wenye historia ya miongo kadhaa. Kuna uwezekano mkubwa pande zote zinatumia muda huu kujipanga upya kimkakati.
Je, wadau mnadhani huu ni ushindi wa Marekani kupitia diplomasia ya ubabe (Coercive diplomacy), au ni ushindi wa Iran kwa kufanikiwa kuiweka Marekani mezani kujadili masharti yao? Na je, hii vita imezimika au ni kalenda tu imesogezwa mbele?
Karibuni kwa mjadala. Wale wataalamu wetu wa Pro-US (wa kambi ya Magharibi) na Pro-Iran (wa kambi ya Mashariki), dondosheni nondo zenu!
=============================
President Donald Trump on Tuesday said he agreed to suspend planned attacks on Iranian infrastructure for two weeks, backing off his shocking threats to imminently order the destruction of Iran's "whole civilization."
The move, more than five weeks after the U.S. and Israel launched the war, was "subject to the Islamic Republic of Iran agreeing to the COMPLETE, IMMEDIATE, and SAFE OPENING of the Strait of Hormuz," he wrote on Truth Social.
The decision was "based on conversations with Prime Minister Shehbaz Sharif and Field Marshal Asim Munir, of Pakistan," Trump wrote.
"This will be a double sided CEASEFIRE!" he declared.
Oil prices plunged as much as 16% following the announcement, while U.S. stock futures shot up.
Iran Foreign Minister Abbas Araghchi said in a separate statement that ships will be able to safely pass through the strait for the two-week interval "via coordination with Iran's Armed Forces and with due consideration of technical limitations."
Trump's announcement came less than two hours before his deadline on Iran to either make a deal that includes opening the strait — a vital artery for global oil transit — or else face major attacks on its civilian infrastructure.
Source: CNBC