Donald Trump amfokea mwandishi na kumwambia 'wewe ni mpumbavu sana'

Atukuzwaye

Senior Member
Joined
Oct 5, 2026
Posts
191
Reaction score
250
Rais Donald Trump amemshambulia kwa maneno mwandishi wa habari wa CNN alipokuwa akitetea uamuzi wake wa kuchelewesha vikwazo dhidi ya Urusi wakati wa mazungumzo yaliyolenga kuhakikisha kuachiwa kwa raia wa Marekani, Stephen Hubbard.

Trump alimwambia mwandishi huyo: “hujui unachozungumza, wewe ni mjinga, una uwezo mdogo wa kufikiri. Na kwa taarifa yako kituo chako ni kibaya kuliko vyote"

Trump alieleza kuwa kuweka vikwazo dhidi ya Urusi wakati mazungumzo hayo yakiendelea kungeweza kuhatarisha mara moja kuachiwa kwa Hubbard. “Kwa hiyo, tumia akili yako,” alimwambia mwandishi huyo.

Wengi wanahoji kuwa Trump amebadilika sana siku hizi mwenendo wake umekua sio wa kawaida yani.

Nipeni maoni yenu wadau wangu kwenye pitapita zenu huko mmekutana na lipi la Trump?😀😀
​
 
View attachment 3695980
marekani angeweza kumjibu na wewe ni mpumbavu kuwahi kuwa rais na asifanywe chochote .....
 
marekan angwea kumjibu na wewe ni mpumbavu kuwahi kuwa rais
Mbona huku Jeiefu tumeshazoea kutukanana makubwa hata zaidi ya hapo?? Kuambiwa mpumbavu tuu!. Sijaona lolote geni hapo. Kwanza ni moja wapo ya sifa kufokewa na Rais wa Taifa kubwa i.e. Amemfagilia.
Kuna tofauti kubwa kati ya kufokewa na kutukanwa.
 
Back
Top Bottom