POTOSHI Donald Trump apigwa na msalaba wakati akihubiri kanisani

POTOSHI Donald Trump apigwa na msalaba wakati akihubiri kanisani

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
1792418315663.png
 
Tunachokijua
Donald John Trump, mwanasiasa, na amehudumu kama Rais wa 45 wa taifa hilo kati ya mwaka 2017 na 2021. Trump anajulikana kwa kuwa rais wa pili katika historia ya Marekani kuchaguliwa tena kwa vipindi viwili visivyofuatana, akirejea madarakani baada ya kushinda uchaguzi wa Novemba 2024.

Madai
Kumekuwepo na video iliyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa X,zamani twitter ikidaiwa kumuonesha Rais wa Marekani, Donald Trump, akihubiri kanisani kabla ya kuangukiwa na msalaba na kuanguka chini.

Video hiyo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuzua maoni mbalimbali miongoni mwa watumiaji wa mitandao hiyo.

Uhalisia

Ufuatiliaji wa kimtandao umebaini kuwa video hiyo imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili unde , kwa kutumia tukio halisi lililotokea hivi karibuni kama rejea.

Tukio hilo lilitokea Jumamosi, Oktoba 17, 2026, katika Kanisa la Nuestra Señora del Perpetuo Socorro, lililopo mjini Guayaquil, nchini Ecuador.

Wakati padre Sánchez akiongoza misa iliyokuwa ikirushwa mubashara kupitia mitandao ya kijamii, msalaba mkubwa wa mbao uliokuwa ukutani nyuma ya madhabahu ulijichomoa ghafla na kumwangukia kichwani na mwilini.

Licha ya waumini kukimbilia kumsaidia na kuitwa kwa gari la wagonjwa, Padre Sánchez alifariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata.

Hivyo, video inayodaiwa kumuonesha Donald Trump akiangukiwa na msalaba kanisani imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili unde, ikitumia tukio hilo halisi kama rejea.
Back
Top Bottom