Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Picha: Chapisho la kwanza la Trump kwenye mtandao wake
Jukwaa la mtandao wa kijamii la Donald Trump, Truth Social limezinduliwa,kwa kiasi kidogo kwenye Apple App store nchini Marekani.
Wachambuzi wamebaini kuwa programu hiyo inafanana na Twitter. Bw Trump alipigwa marufuku kutoka Twitter, Facebook na YouTube mwaka jana.
Na watumiaji wengine wa mapema walikuwa na shida kusajili akaunti.
Kiongozi wa mradi na mbunge wa zamani Devin Nunes alisema unatarajiwa kufanya kazi kikamilifu mwishoni mwa Machi.
Baadhi ya wale wanaojaribu kujiandikisha walikuwa wameambiwa: "Kwa sababu ya mahitaji makubwa, tumekuweka kwenye orodha yetu ya wanaosubiri," shirika la habari la Reuters liliripoti.
Imeundwa na kampuni ya Trump Media & Technology Group (TMTG), Truth Social hapo awali ilitolewa kwa watumiaji wapatao 500 wanaojaribu beta.
Wiki iliyopita, Donald Trump Jr aliweka mtandaoni picha ya skrini ya "ukweli" wa kwanza wa baba yake kwenye mtandao wa kijamii: "Jitayarishe. Rais wako unayempenda atakuona hivi karibuni." Aliandika .