Donald Trump aridhia kuanza kwa mchakato wa kumkabidhi madaraka Joe Biden

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Donald Trump ametangaza mapema Jumatatu jioni, Novemba 24, kwamba ameridhia ufunguzi wa mchakato wa kumkabidhi madaraka mrithi wake Joe Biden kutoka chama cha Democratic, zaidi ya wiki mbili baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais.

Idara ya serikali ya Marekani inayoratibu shughuli ya kubadilishana madaraka, imempatia rais mteule Joe Biden idhini ya kuendelea na mchakato wa kukabidhiana madaraka huku Trump naye akionekana kukubali kutoa ushirikiano.

Trump amekiri kuwa umefika muda sasa kwa taasisi hiyo kufanya "kinachohitajika" na kaandika katika Twitta kwamba ameielekeza timu yake kutoa ushirikiano katika mchakato wa kukabidhiana madaraka.

Wakati huo huo Timu ya Bwana Biden imefurahishwa na kuanza kwa mchakato huo wakati rais mteule anajiandaa katika sherehe za kuapishwa Januari 20.

Rais anayemaliza muda wake Donald Trump kutoka chama cha wa Republican, hata hivyo, amejizuia kutambua moja kwa moja ushindi wa Joe Biden, huku akiahidi kuendelea na "mapambano ya haki" wakati anaendelea kuwasilisha malalamiko yake mbele ya mahakama mbalimbali nchini humo, bila mafanikio yoyote, kujaribu kuonyesha udanganyifu wakati wa uchaguzi wa urais wa Novemba 3 .

Ofisi ya utawala wa huduma za serikali imesema inamtambua Bwana Biden kama "mshindi".
 
Attachments

  • IMG-20201122-WA0012.jpg
    IMG-20201122-WA0012.jpg
    54.2 KB · Views: 2
Tanzania muliapisha mbio mbio mkatangaza serikali na Lissu mgombea urais akatishiwa maisha, Lema yupo ukimbizini Kenya, watu wameauwawa wengine majeraha kina jussa, vifaru na ndege za kivita na majeshi kukodiwa toka burundi
 
Hata asingeridhia angeondoka tu maana democracy iliyopo USA sio kama sehemu nyinginezo za ulimwengu.
 
Tanzania muliapisha mbio mbio mkatangaza serikali na Lissu mgombea urais akatishiwa maisha, Lema yupo ukimbizini Kenya, watu wameauwawa wengine majeraha kina jussa, vifaru na ndege za kivita na majeshi kukodiwa toka burundi
What?
 
Babu Trump anajiandaa kuondoka ikulu hapo mwakani.
 
Donald Trump ametangaza mapema Jumatatu jioni, Novemba 24, kwamba ameridhia ufunguzi wa mchakato wa kumkabidhi madaraka mrithi wake Joe Biden kutoka chama cha Democratic, zaidi ya wiki mbili baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais.

Idara ya serikali ya Marekani inayoratibu shughuli ya kubadilishana madaraka, imempatia rais mteule Joe Biden idhini ya kuendelea na mchakato wa kukabidhiana madaraka huku Trump naye akionekana kukubali kutoa ushirikiano.

Trump amekiri kuwa umefika muda sasa kwa taasisi hiyo kufanya "kinachohitajika" na kaandika katika Twitta kwamba ameielekeza timu yake kutoa ushirikiano katika mchakato wa kukabidhiana madaraka.

Wakati huo huo Timu ya Bwana Biden imefurahishwa na kuanza kwa mchakato huo wakati rais mteule anajiandaa katika sherehe za kuapishwa Januari 20.

Rais anayemaliza muda wake Donald Trump kutoka chama cha wa Republican, hata hivyo, amejizuia kutambua moja kwa moja ushindi wa Joe Biden, huku akiahidi kuendelea na "mapambano ya haki" wakati anaendelea kuwasilisha malalamiko yake mbele ya mahakama mbalimbali nchini humo, bila mafanikio yoyote, kujaribu kuonyesha udanganyifu wakati wa uchaguzi wa urais wa Novemba 3 .

Ofisi ya utawala wa huduma za serikali imesema inamtambua Bwana Biden kama "mshindi".
Ana vituko tramp
 
BIDDEN AMEMTEUA LLYOD AUSTIN KUWA CHIEF SECRETARY OF DEFENCE...KUTOKA KWA TRUMP SIO HIARI NI AMRI ILA NIMPENDA SIFA TU KWA HIYO LAZIMA
 
Back
Top Bottom