Donald Trump: Tutaiongoza Venezuela hadi Serikali ya Wananchi itakapopatikana

Donald Trump: Tutaiongoza Venezuela hadi Serikali ya Wananchi itakapopatikana

Kuna faida gani kuwa na rais kama dikteta Nicolus Maduri kama raia zaidi ya milioni saba wa Venezuela wamekimbia udikteta wake na wanaishi uhamishoni.

Kila siku tunasema kwamba madikteta huua uzalendo ona sasa Maduro anachukuliwa mithili ya kichuchu anayechukuliwa na mwewe tena kwenye ikulu iliyo karibu kabisa na kambi ya jeshi na wanajeshi wasifanye chochote.

Lakini shida ya madikteta ni kwamba sio watu wa kujifunza, hata kidogo na sasa wananchi wa Venezuela wataona heri kutawaliwa na nchi ya kigeni kuliko mwananchi mwenzao muuaji hapa Samia ana somo kubwa sana ya kujifunza.
 
Back
Top Bottom